Utafanya upatanisho kwa ajili ya hiyo madhabahu muda wa siku saba, na kuitakasa; ndipo madhabahu itakapokuwa takatifu sana; kila kitu kiigusacho madhabahu kitakuwa kitakatifu.
Walawi 6:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kila kitu kitakachoigusa nyama ya sadaka hiyo kitakuwa kitakatifu; tena itakapomwagika damu yake yeyote katika nguo yoyote, utaifua nguo hiyo iliyomwagiwa, katika mahali patakatifu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Chochote kitakachogusa nyama hiyo kitakuwa kitakatifu; vazi lolote likidondokewa na damu ya sadaka hiyo, basi, vazi hilo litaoshewa mahali patakatifu. Biblia Habari Njema - BHND Chochote kitakachogusa nyama hiyo kitakuwa kitakatifu; vazi lolote likidondokewa na damu ya sadaka hiyo, basi, vazi hilo litaoshewa mahali patakatifu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Chochote kitakachogusa nyama hiyo kitakuwa kitakatifu; vazi lolote likidondokewa na damu ya sadaka hiyo, basi, vazi hilo litaoshewa mahali patakatifu. Neno: Bibilia Takatifu Chochote kitakachogusa nyama yoyote ya hiyo sadaka kitakuwa kitakatifu; na kama damu ya hiyo sadaka itadondokea juu ya vazi, lazima ulifulie mahali patakatifu. Neno: Maandiko Matakatifu Chochote kitakachogusa nyama yoyote ya hiyo sadaka kitakuwa kitakatifu, na kama hiyo damu itadondokea juu ya vazi, lazima uifulie mahali patakatifu. BIBLIA KISWAHILI Kila kitu kitakachoigusa nyama ya sadaka hiyo kitakuwa kitakatifu; tena itakapomwagika damu yake yeyote katika nguo yoyote, utaifua nguo hiyo iliyomwagiwa, katika mahali patakatifu. |
Utafanya upatanisho kwa ajili ya hiyo madhabahu muda wa siku saba, na kuitakasa; ndipo madhabahu itakapokuwa takatifu sana; kila kitu kiigusacho madhabahu kitakuwa kitakatifu.
Nawe utavitakasa vitu hivyo, ili viwe vitakatifu sana; tena kila kivigusacho vyombo vile kitakuwa kitakatifu.
Nao watakapotoka kuingia ua wa nje, yaani, ua wa nje wa watu, ndipo watakapoyavua mavazi yao waliyovaa katika huduma yao, na kuyaweka katika vile vyumba vitakatifu, nao watavaa mavazi mengine, wasije wakawatakasa watu kwa mavazi yao.
Tena kitu chochote, wanyama hao mmojawapo atakachokiangukia, wakiisha kufa, kitakuwa ni najisi; cha mti, nguo, ngozi, gunia, chombo chochote cha kufanyia kazi yoyote, lazima kitiwe ndani ya maji, nacho kitakuwa ni najisi hadi jioni; ndipo kitakapokuwa ni safi.
Kila mwanamume miongoni mwa wana wa Haruni atakula katika huo, kuwa ni haki yao milele katika vizazi vyenu, katika matoleo ya BWANA yasongezwayo kwa njia ya moto; mtu yeyote atakayevigusa atakuwa ni mtakatifu.
Tena nyama itakayogusa kitu kilicho najisi haitaliwa; itachomwa moto. Na katika hiyo nyama nyingine, kila mtu aliye safi ana ruhusa kuila;
Mtu akichukua nyama takatifu katika upindo wa nguo yake, naye kwa upindo wake akagusa mkate, au ugali, au divai, au mafuta, au chakula chochote, je, Kitu hicho kitakuwa kitakatifu? Makuhani wakajibu, wakasema, La.
Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu kutoka kwa uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu.
Maana, angalieni, kuhuzunishwa kuko huko kwa jinsi ya Mungu kulitenda bidii gani ndani yenu; naam, na kujitetea, naam, na kukasirika, naam, na hofu, naam, na shauku, naam, na kujitahidi, naam, na kisasi! Kwa kila njia mmejionesha wenyewe kuwa safi katika jambo hilo.