kisha atamnyunyizia huyo atakayetakaswa na ukoma mara saba, naye atasema kwamba ni safi, kisha atamwacha yule ndege aliye hai aende zake nyikani.
Walawi 4:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC kisha kuhani atatia kidole chake katika hiyo damu, na kuinyunyiza mbele za BWANA, mbele ya pazia mara saba. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Atachovya kidole chake katika hiyo damu na kuinyunyiza mbele ya pazia mara saba, mbele ya Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Atachovya kidole chake katika hiyo damu na kuinyunyiza mbele ya pazia mara saba, mbele ya Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Atachovya kidole chake katika hiyo damu na kuinyunyiza mbele ya pazia mara saba, mbele ya Mwenyezi-Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Atachovya kidole chake kwenye damu na kuinyunyiza mara saba mbele za Mwenyezi Mungu mbele ya hilo pazia. Neno: Maandiko Matakatifu Atachovya kidole chake kwenye damu na kuinyunyiza mara saba mbele za bwana mbele ya hilo pazia. BIBLIA KISWAHILI kisha kuhani atatia kidole chake katika hiyo damu, na kuinyunyiza mbele za BWANA, mbele ya pazia mara saba. |
kisha atamnyunyizia huyo atakayetakaswa na ukoma mara saba, naye atasema kwamba ni safi, kisha atamwacha yule ndege aliye hai aende zake nyikani.
Kisha atatwaa baadhi ya damu ya yule ng'ombe, na kuinyunyiza kwa kidole chake juu ya kiti cha rehema upande wa mashariki; na mbele ya kiti cha rehema atainyunyiza ile damu kwa kidole chake mara saba.
kisha ng'ombe atachinjwa mbele za BWANA. Kisha kuhani aliyetiwa mafuta atatwaa baadhi ya damu ya huyo ng'ombe na kuileta ndani ya hema ya kukutania;
Kisha huyo kuhani aliyetiwa mafuta atatwaa baadhi ya damu ya huyo ng'ombe, na kuileta ndani ya hiyo hema ya kukutania;
Kisha akanyunyiza hayo mafuta juu ya madhabahu mara saba, na kuitia mafuta madhabahu na vyombo vyake vyote, na birika na kitako chake, ili kuvitakasa.
kisha Eleazari kuhani atatwaa katika damu yake kwa kidole chake, na kuinyunyiza damu yake kuelekea upande wa mbele wa hema ya kukutania mara saba;