Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Walawi 27:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Na kama ni wa mnyama asiye safi, ndipo atamkomboa kama hesabu yako ilivyo, naye ataongeza sehemu ya tano ya bei yake; au asipokombolewa, ndipo atauzwa kama hesabu yako ilivyo.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Kama anayehusika ni mnyama najisi, mwenyewe atamnunua kwa kulingana na mnavyompima na ataongeza asilimia ishirini ya thamani ya mnyama huyo. Kama hakombolewi, basi, atauzwa kulingana na vipimo vyenu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Kama anayehusika ni mnyama najisi, mwenyewe atamnunua kwa kulingana na mnavyompima na ataongeza asilimia ishirini ya thamani ya mnyama huyo. Kama hakombolewi, basi, atauzwa kulingana na vipimo vyenu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Kama anayehusika ni mnyama najisi, mwenyewe atamnunua kwa kulingana na mnavyompima na ataongeza asilimia ishirini ya thamani ya mnyama huyo. Kama hakombolewi, basi, atauzwa kulingana na vipimo vyenu.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Kama ni mmoja wa wanyama walio najisi, aweza kumnunua kwa bei iliyowekwa, akiongeza sehemu ya tano ya thamani yake. Kama hatamkomboa, mnyama huyo atauzwa kwa bei iliyowekwa.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Kama ni mmoja wa wanyama walio najisi, aweza kumnunua kwa bei iliyowekwa, akiongeza sehemu ya tano ya thamani yake. Kama hatamkomboa, mnyama huyo atauzwa kwa bei iliyowekwa.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Na kama ni wa mnyama asiye safi, ndipo atamkomboa kama hesabu yako ilivyo, naye ataongeza sehemu ya tano ya bei yake; au asipokombolewa, ndipo atauzwa kama hesabu yako ilivyo.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Walawi 27:27
7 Marejeleo ya Msalaba  

Na kama ni mnyama yeyote asiye safi, wa namna ambayo hawamsongezi kwa BWANA, basi atamweka huyo mnyama mbele ya kuhani;

Lakini kwamba ataka kumkomboa kweli, ndipo atakapoongeza sehemu ya tano juu ya hesabu yako.

Tena mtu huyo aliyeweka nyumba yake iwe wakfu kama akitaka kuikomboa, ndipo atakapoongeza sehemu ya tano ya hiyo fedha ya hesabu yako, nayo itakuwa mali yake.

Mzaliwa wa kwanza tu katika wanyama, aliyewekwa kuwa mzaliwa wa kwanza kwa BWANA, mtu yeyote hatamweka kuwa mtakatifu; kama ni ng'ombe, kama ni kondoo, huyo ni wa BWANA.

Pamoja na hayo, hakitauzwa wala kukombolewa kitu chochote kilichowekwa wakfu, ambacho mtu amekiweka wakfu kwa BWANA, katika vitu vyote alivyo navyo, kama ni mtu, au mnyama, au kama ni shamba la milki yake; kila kitu kilichowekwa wakfu ni kitakatifu sana kwa BWANA.

Na kama mtu akitaka kukomboa chochote cha zaka yake, ataongeza sehemu yake ya tano juu yake.

naye atalipa kwa ajili ya hilo alilolikosa katika kitu kile kitakatifu, kisha ataongeza na sehemu ya tano, na kumpa kuhani; naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa huyo kondoo dume wa sadaka ya hatia, naye atasamehewa.