Walawi 27:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mwaka wa jubilii shamba hilo litarejea kwake huyo ambaye lilinunuliwa kwake, yaani, huyo ambaye nchi hiyo ni milki yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini katika mwaka wa ukumbusho wa miaka hamsini, shamba hilo ni lazima arudishiwe yule mtu aliyeliuza. Biblia Habari Njema - BHND Lakini katika mwaka wa ukumbusho wa miaka hamsini, shamba hilo ni lazima arudishiwe yule mtu aliyeliuza. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini katika mwaka wa ukumbusho wa miaka hamsini, shamba hilo ni lazima arudishiwe yule mtu aliyeliuza. Neno: Bibilia Takatifu Katika Mwaka wa Yubile, shamba litarudishwa kwa mtu yule ambaye lilinunuliwa kutoka kwake, yule ambaye ardhi ilikuwa mali yake. Neno: Maandiko Matakatifu Katika Mwaka wa Yubile, shamba litarudishwa kwa mtu yule ambaye lilinunuliwa kutoka kwake, yule ambaye ardhi ilikuwa mali yake. BIBLIA KISWAHILI Mwaka wa jubilii shamba hilo litarejea kwake huyo ambaye lilinunuliwa kwake, yaani, huyo ambaye nchi hiyo ni milki yake. |
Lakini asipoweza kujipatia mwenyewe, ndipo hiyo iliyouzwa itakaa mkononi mwake huyo aliyeinunua, hadi mwaka wa jubilii; na katika jubilii ataliachilia, naye mwenyewe atairejea milki yake.
Lakini asipotaka kulikomboa shamba, au kama amemwuzia mtu mwingine hilo shamba, halitakombolewa tena kabisa;
ndipo kuhani atamhesabia kima cha kuhesabu kwako hata mwaka wa jubilii: naye atatoa siku hiyo kama hesabu yako, kuwa ni kitu kitakatifu kwa BWANA.
Na hesabu zako zote zitaandamana shekeli ya mahali patakatifu; gera ishirini zitakuwa shekeli moja.