Na mwaka wa hamsini mtautakasa, na kuwatangazia uhuru watu wote katika nchi; itakuwa ni mwaka wa jubilii kwenu; na kila mtu atairudia milki yake, na kila mtu atarejea kwa jamaa yake.
Walawi 27:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ikiwa anaweka shamba lake liwe wakfu tangu mwaka wa jubilii, litakadiriwa vivyo hivyo kama hesabu yako ilivyo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kama akiliweka wakfu shamba lake katika mwaka wa kuadhimisha miaka hamsini, thamani yake ni lazima ilingane na vipimo vyenu. Biblia Habari Njema - BHND Kama akiliweka wakfu shamba lake katika mwaka wa kuadhimisha miaka hamsini, thamani yake ni lazima ilingane na vipimo vyenu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kama akiliweka wakfu shamba lake katika mwaka wa kuadhimisha miaka hamsini, thamani yake ni lazima ilingane na vipimo vyenu. Neno: Bibilia Takatifu Akiweka shamba lake wakfu katika Mwaka wa Yubile, ile thamani iliyokwisha wekwa itakuwa hiyo hiyo. Neno: Maandiko Matakatifu Kama akiweka shamba lake wakfu katika Mwaka wa Yubile, ile thamani iliyokwisha wekwa itakuwa iyo hiyo. BIBLIA KISWAHILI Ikiwa anaweka shamba lake liwe wakfu tangu mwaka wa jubilii, litakadiriwa vivyo hivyo kama hesabu yako ilivyo. |
Na mwaka wa hamsini mtautakasa, na kuwatangazia uhuru watu wote katika nchi; itakuwa ni mwaka wa jubilii kwenu; na kila mtu atairudia milki yake, na kila mtu atarejea kwa jamaa yake.
Mwaka huo wa hamsini utakuwa ni jubilii kwenu; msipande mbegu, wala msivune kitu hicho kimeacho chenyewe, wala msizitunde zabibu za mizabibu isiyopelewa.
Ndipo utakapoipeleka pande zote hiyo baragumu yenye sauti kuu, siku ya kumi ya mwezi wa saba; katika siku hiyo ya upatanisho mtaipeleka baragumu katika nchi yenu yote.
Na mtu atakapoiweka nyumba yake iwe wakfu kwa BWANA ndipo kuhani ataihesabu kima chake hiyo nyumba, ikiwa njema ikiwa mbaya; kama kuhani atakavyoihesabu kima chake ndivyo itakavyokuwa.
Tena kama mtu akiweka wakfu kwa BWANA sehemu ya shamba la milki yake, ndipo hesabu yako itakuwa kama kule kupanda kwake kulivyo; kupanda kwake homeri moja ya mbegu ya shayiri, kutahesabiwa kuwa ni shekeli hamsini za fedha.
Lakini akiliweka shamba lake wakfu baada ya jubilii, ndipo kuhani atamhesabia hiyo fedha kama hesabu ya miaka iliyobaki hata mwaka wa jubilii, na kuhesabiwa kwako kutapunguzwa.