Tena itakuwa katika siku hiyo, tarumbeta kubwa itapigwa, nao waliokuwa karibu kuangamia katika nchi ya Ashuru watakuja; na hao waliotupwa katika nchi ya Misri; nao watamsujudu BWANA katika mlima mtakatifu huko Yerusalemu.
Walawi 26:38 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nanyi mtaangamia kati ya mataifa, na nchi ya adui zenu itawameza. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtaangamia kati ya mataifa na nchi za adui zenu zitawameza. Biblia Habari Njema - BHND Mtaangamia kati ya mataifa na nchi za adui zenu zitawameza. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtaangamia kati ya mataifa na nchi za adui zenu zitawameza. Neno: Bibilia Takatifu Mtaangamia kati ya mataifa; nchi ya adui zenu itawala. Neno: Maandiko Matakatifu Mtaangamia katikati ya mataifa; nchi ya adui zenu itawala. BIBLIA KISWAHILI Nanyi mtaangamia kati ya mataifa, na nchi ya adui zenu itawameza. |
Tena itakuwa katika siku hiyo, tarumbeta kubwa itapigwa, nao waliokuwa karibu kuangamia katika nchi ya Ashuru watakuja; na hao waliotupwa katika nchi ya Misri; nao watamsujudu BWANA katika mlima mtakatifu huko Yerusalemu.
bali katika mahali pale walipomchukua mateka ndipo atakapokufa, wala hataiona nchi hii tena kamwe.
Basi, sasa jueni sana ya kuwa mtakufa kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni, katika mahali pale mnapopatamani kwenda na kukaa.
Na watu wa kwenu watakaobaki watafifia kwa ajili ya uovu wao, katika hizo nchi za adui zenu; tena watafifia kwa ajili ya uovu wa baba zao, pamoja nao.
kwa hiyo utawatumikia adui zako atakaowaleta BWANA juu yako, kwa njaa, na kwa kiu, na kwa uchi, na kwa uhitaji wa vitu vyote; naye atakuvika kongwa la chuma shingoni mwako, hata atakapokwisha kukuangamiza.
BWANA atakurudisha tena Misri kwa merikebu, kwa njia ambayo nilikuambia, Hutaiona tena popote; nanyi huko mtajiuza nafsi zenu kwa adui zenu kuwa watumwa na wajakazi, wala hapana atakayewanunua.