Na kama mtu hana atakayeikomboa, naye mwenyewe amepata mali na kujiona kuwa anayo ya kutosha kuikomboa;
Walawi 25:49 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC au mjomba wake, au mwana wa mjomba wake, ana ruhusa ya kumkomboa, au mtu yeyote aliye karibu naye wa jamaa yake, ana ruhusa ya kumkomboa; au kama yeye mwenyewe amepata mali, ana ruhusa ya kujikomboa mwenyewe. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mjomba wake anaweza pia kumkomboa, au binamu yake au ndugu wa karibu katika ukoo wake; anaweza pia kujikomboa yeye mwenyewe kama akiwa tajiri. Biblia Habari Njema - BHND Mjomba wake anaweza pia kumkomboa, au binamu yake au ndugu wa karibu katika ukoo wake; anaweza pia kujikomboa yeye mwenyewe kama akiwa tajiri. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mjomba wake anaweza pia kumkomboa, au binamu yake au ndugu wa karibu katika ukoo wake; anaweza pia kujikomboa yeye mwenyewe kama akiwa tajiri. Neno: Bibilia Takatifu Mjomba wake, au binamu yake, au yeyote aliye ndugu wa damu katika ukoo wake aweza kumkomboa. Au akifanikiwa, anaweza kujikomboa mwenyewe. Neno: Maandiko Matakatifu Mjomba wake, au binamu yake, au yeyote aliye ndugu wa damu katika ukoo wake aweza kumkomboa. Au ikiwa atafanikiwa, anaweza kujikomboa mwenyewe. BIBLIA KISWAHILI au mjomba wake, au mwana wa mjomba wake, ana ruhusa ya kumkomboa, au mtu yeyote aliye karibu naye wa jamaa yake, ana ruhusa ya kumkomboa; au kama yeye mwenyewe amepata mali, ana ruhusa ya kujikomboa mwenyewe. |
Na kama mtu hana atakayeikomboa, naye mwenyewe amepata mali na kujiona kuwa anayo ya kutosha kuikomboa;
ndipo na aihesabu hiyo miaka ya kuuzwa kwake, na kilichozidi kumrudishia huyo mtu aliyeinunua; naye atairejea milki yake.
baada ya kuuzwa aweza kukombolewa; mtu mmoja miongoni mwa ndugu zake ana ruhusa kumkomboa;
Naye atafanya hesabu na huyo aliyemnunua, tangu mwaka huo aliojiuza hata mwaka wa jubilii; na ile bei ya kuuzwa kwake itakuwa kama hesabu ya hiyo miaka ilivyo; atakuwa pamoja naye kama majira ya mtumishi aliyeajiriwa yalivyo.