lakini mtumishi wa mtu awaye yote aliyenunuliwa kwa fedha, ukiisha kumtahiri, ndipo hapo atamla Pasaka.
Walawi 25:44 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Tena kuhusu watumishi wako na wajakazi wako, utakaokuwa nao; mataifa walio kando yenu, katika hao mtanunua watumishi na wajakazi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kuhusu watumwa, wa kike na wa kiume, unaweza kuwanunua kutoka kwa watu wa mataifa mengine ya jirani. Biblia Habari Njema - BHND Kuhusu watumwa, wa kike na wa kiume, unaweza kuwanunua kutoka kwa watu wa mataifa mengine ya jirani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kuhusu watumwa, wa kike na wa kiume, unaweza kuwanunua kutoka kwa watu wa mataifa mengine ya jirani. Neno: Bibilia Takatifu “ ‘Watumwa wako wa kiume na wa kike watatoka katika mataifa yanayokuzunguka; unaweza kununua watumwa kutoka kwao. Neno: Maandiko Matakatifu “ ‘Watumwa wako wa kiume na wa kike watatoka katika mataifa yanayokuzunguka; kutoka kwao waweza kununua watumwa. BIBLIA KISWAHILI Tena kuhusu watumishi wako na wajakazi wako, utakaokuwa nao; mataifa walio kando yenu, katika hao mtanunua watumishi na wajakazi. |
lakini mtumishi wa mtu awaye yote aliyenunuliwa kwa fedha, ukiisha kumtahiri, ndipo hapo atamla Pasaka.
Tena wana wa wageni wakaao kati yenu mtajinunulia, na katika jamaa zao walio pamoja nanyi, waliowazaa katika nchi yenu; wao watakuwa milki yenu.