Kutangaza mwaka wa BWANA uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao;
Walawi 25:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mwaka huo wa jubilii mtairudia kila mtu milki yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Katika mwaka huo chochote ambacho kiliuzwa ni lazima kirudishwe kwa mwenyewe. Biblia Habari Njema - BHND “Katika mwaka huo chochote ambacho kiliuzwa ni lazima kirudishwe kwa mwenyewe. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Katika mwaka huo chochote ambacho kiliuzwa ni lazima kirudishwe kwa mwenyewe. Neno: Bibilia Takatifu “ ‘Katika huu Mwaka wa Yubile, kila mmoja atarudi kwenye mali yake mwenyewe. Neno: Maandiko Matakatifu “ ‘Katika huu Mwaka wa Yubile, kila mmoja atarudi kwenye mali yake mwenyewe. BIBLIA KISWAHILI Mwaka huo wa jubilii mtairudia kila mtu milki yake. |
Kutangaza mwaka wa BWANA uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao;
Kwa maana auzaye hatakirudia kilichouzwa, wajapokuwa wangali hai; kwa sababu maono haya yawahusu watu wote; hapana mmoja atakayerudi; wala hapana mtu atakayejitia nguvu katika uovu wa maisha yake.
Na mwaka wa hamsini mtautakasa, na kuwatangazia uhuru watu wote katika nchi; itakuwa ni mwaka wa jubilii kwenu; na kila mtu atairudia milki yake, na kila mtu atarejea kwa jamaa yake.
Kwa kuwa ni jubilii; utakuwa mwaka mtakatifu kwenu; mtakula mavuno yake yatokayo shambani.
Lakini asipoweza kujipatia mwenyewe, ndipo hiyo iliyouzwa itakaa mkononi mwake huyo aliyeinunua, hadi mwaka wa jubilii; na katika jubilii ataliachilia, naye mwenyewe atairejea milki yake.
Tena kwamba hakukombolewa kwa njia mojawapo ya hizi, ndipo atatoka katika mwaka wa jubilii, yeye, pamoja na watoto wake.
Tena itakapokuwapo hiyo jubilii ya wana wa Israeli, ndipo urithi wa hilo kabila ambalo wamekuwa ndani yake utaongezewa huo urithi wao; hivyo urithi wao utaondolewa katika urithi wa kabila la baba zetu.