na vinara vya taa, vitano upande wa kulia, na vitano upande wa kushoto, mbele ya chumba cha ndani, vya dhahabu safi; na maua, na taa, na koleo ya dhahabu;
Walawi 24:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Atazitengeneza hizo taa katika kile kinara kilicho safi mbele za BWANA daima. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ataziweka hizo taa katika kinara cha taa cha dhahabu safi ziwake daima mbele ya Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Ataziweka hizo taa katika kinara cha taa cha dhahabu safi ziwake daima mbele ya Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ataziweka hizo taa katika kinara cha taa cha dhahabu safi ziwake daima mbele ya Mwenyezi-Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Taa zilizo juu ya kinara cha dhahabu safi mbele za Mwenyezi Mungu lazima zihudumiwe daima. Neno: Maandiko Matakatifu Taa zilizo juu ya kinara cha dhahabu safi mbele za bwana lazima zihudumiwe daima. BIBLIA KISWAHILI Atazitengeneza hizo taa katika kile kinara kilicho safi mbele za BWANA daima. |
na vinara vya taa, vitano upande wa kulia, na vitano upande wa kushoto, mbele ya chumba cha ndani, vya dhahabu safi; na maua, na taa, na koleo ya dhahabu;
kwa uzani tena kwa vinara vya dhahabu, na kwa taa zake za dhahabu, kwa uzani, kwa kila kinara, na kwa taa zake; na kwa vinara vya fedha, kwa uzani kwa kila kinara na kwa taa zake, kwa kadiri ya matumizi ya kila kinara;
Tena wameifunga milango ya ukumbi, na kuzizima taa, wala hawakufukiza uvumba, wala hawakumtolea Mungu wa Israeli sadaka za kuteketezwa katika patakatifu.
na meza, na vyombo vyake, na kinara cha taa safi pamoja na vyombo vyake vyote, na madhabahu ya kufukizia uvumba;
na kinara cha taa safi, na taa zake, hizo taa za kuwekwa mahali pake, na vyombo vyake vyote, na mafuta ya taa,
Navyo vikombe, na vyombo vya kutolea majivu, na mabakuli, na masufuria, na vinara, na miiko, na vyetezo, vilivyokuwa vya dhahabu katika dhahabu, na vilivyokuwa vya fedha katika fedha, kamanda wa askari walinzi akavichukua.
Hapo nje ya pazia la ushahidi, ndani ya hema ya kukutania, Haruni ataitengeneza tangu jioni hadi asubuhi mbele za BWANA daima; ni amri ya milele katika vizazi vyenu.
Na vitu watakavyovitunza ni hilo sanduku, na meza, na kinara cha taa, na madhabahu, na vile vyombo vya mahali patakatifu wavitumiavyo katika huduma yao, na pazia, na utumishi wake wote.
Kisha watatwaa nguo ya rangi ya samawati, na kukifunika kinara cha taa ya nuru, na taa zake, na makasi yake, na sahani zake za kuwekea makaa, na vyombo vyake vyote vya mafuta, watumiavyo kwa kazi yake;
Nena na Haruni, ukamwambie, Utakapoziweka taa, hizo taa saba zitatoa nuru hapo mbele ya kinara cha taa.
Maana hema ilitengenezwa, ile ya kwanza, mlimokuwa na kinara cha taa, na meza, na mikate mitakatifu; ndipo palipoitwa, Patakatifu.
Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kulia, na ya vile vinara saba vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni makanisa saba.
Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.