Walawi 24:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mtakuwa na sheria moja tu, kwa huyo aliye mgeni, na kwa mzalia; kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sheria hii yamhusu mgeni na mwenyeji. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.” Biblia Habari Njema - BHND Sheria hii yamhusu mgeni na mwenyeji. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sheria hii yamhusu mgeni na mwenyeji. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.” Neno: Bibilia Takatifu Mtakuwa na sheria hiyo hiyo kwa mgeni na kwa mzawa. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu.’ ” Neno: Maandiko Matakatifu Mtakuwa na sheria iyo hiyo kwa mgeni na kwa mzawa. Mimi ndimi bwana Mwenyezi Mungu wenu.’ ” BIBLIA KISWAHILI Mtakuwa na sheria moja tu, kwa huyo aliye mgeni, na kwa mzaliwa; kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. |
Kisha mtu yeyote wa nyumba ya Israeli, au miongoni mwa hao wageni wakaao kati yao, atakayekula damu, ya aina yoyote, nitamkataa mtu huyo alaye damu, na nitamtenga na watu wake.
Mgeni aishiye pamoja nawe atakuwa kama mzaliwa kwenu; mpende kama nafsi yako; kwa maana ninyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri; Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
Musa akanena na wana wa Israeli, nao wakamtoa huyo aliyeapiza nje ya kambi, wakamwua kwa kumpiga kwa mawe. Wana wa Israeli wakafanya kama BWANA alivyomwagiza Musa.
Mtakuwa na sheria moja kwa huyo afanyaye neno lolote pasipo kujua, kwa huyo aliyezaliwa kwenu kati ya wana wa Israeli, na kwa mgeni akaaye kati yao.
Na kama mgeni akiketi kati yenu ugenini, naye ataka kuishika Pasaka kwa BWANA; kama hiyo sheria ya Pasaka ilivyo, na kama amri yake ilivyo, ndivyo atakavyofanya; mtakuwa na sheria moja, kwa huyo aliye mgeni, na kwa huyo aliyezaliwa katika nchi.
Nikawaagiza wakati ule waamuzi wenu, nikawaambia, Sikilizeni ninyi maneno kati ya ndugu zenu, mkaamue kwa haki kati ya mtu na nduguye, na mgeni aliye pamoja naye.