mkawaketishe watu wawili, watu walaghai, ili wamshitaki, na kumshuhudia, kunena, Umemtukana Mungu na mfalme. Kisha mchukueni nje, mkampige kwa mawe, ili afe.
Walawi 24:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nawe nena na wana wa Israeli na kuwaambia, Mtu yeyote atakayemlaani Mungu wake atachukua dhambi yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nawe uwaambie Waisraeli kwamba mtu yeyote atakayemlaani Mungu wake ni lazima awajibike kwa dhambi yake. Biblia Habari Njema - BHND Nawe uwaambie Waisraeli kwamba mtu yeyote atakayemlaani Mungu wake ni lazima awajibike kwa dhambi yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nawe uwaambie Waisraeli kwamba mtu yeyote atakayemlaani Mungu wake ni lazima awajibike kwa dhambi yake. Neno: Bibilia Takatifu Waambie Waisraeli: ‘Ikiwa mtu yeyote atamlaani Mungu wake, atakuwa na hatia kwa uovu wake. Neno: Maandiko Matakatifu Waambie Waisraeli: ‘Ikiwa mtu yeyote atamlaani Mungu wake, atakuwa na hatia kwa uovu wake; BIBLIA KISWAHILI Nawe nena na wana wa Israeli na kuwaambia, Mtu yeyote atakayemlaani Mungu wake atachukua dhambi yake. |
mkawaketishe watu wawili, watu walaghai, ili wamshitaki, na kumshuhudia, kunena, Umemtukana Mungu na mfalme. Kisha mchukueni nje, mkampige kwa mawe, ili afe.
Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.
Usimtoe kafara mzawa wako yeyote kwa Moleki na ulinajisi jina la Mungu wako; mimi ndimi BWANA.
Na mtu yeyote akifanya dhambi, kwa kuwa ameisikia sauti yenye kuapisha, naye akawa ni shahidi, kwamba aliona au kujua, asipolifunua neno lile, ndipo atakapochukua uovu wake mwenyewe;
Lakini mtu aliye safi, wala hakuwa katika safari, naye amekosa kuishika Pasaka, mtu huyo atatengwa na watu wake; kwa sababu hakumtolea BWANA matoleo kwa wakati wake ulioamriwa, mtu huyo atachukua dhambi yake.