mkawaketishe watu wawili, watu walaghai, ili wamshitaki, na kumshuhudia, kunena, Umemtukana Mungu na mfalme. Kisha mchukueni nje, mkampige kwa mawe, ili afe.
Walawi 24:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mtoe huyo aliyelaani nje ya kambi; na wale wote waliomsikia na waweke mikono yao kichwani mwake, kisha mkutano wote na wamwue kwa kumpiga kwa mawe. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Mtoe kijana aliyekufuru nje ya kambi, na wale wote waliomsikia akikufuru waweke mikono yao juu ya kichwa chake, na jumuiya yote imuue kwa kumpiga mawe. Biblia Habari Njema - BHND “Mtoe kijana aliyekufuru nje ya kambi, na wale wote waliomsikia akikufuru waweke mikono yao juu ya kichwa chake, na jumuiya yote imuue kwa kumpiga mawe. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Mtoe kijana aliyekufuru nje ya kambi, na wale wote waliomsikia akikufuru waweke mikono yao juu ya kichwa chake, na jumuiya yote imuue kwa kumpiga mawe. Neno: Bibilia Takatifu “Mchukue huyo aliyekufuru nje ya kambi. Wale wote waliomsikia akikufuru wataweka mikono juu ya kichwa chake, kisha kusanyiko lote watampiga mawe. Neno: Maandiko Matakatifu “Mchukue huyo aliyekufuru nje ya kambi. Wale wote waliomsikia akikufuru wataweka mikono juu ya kichwa chake, kisha kusanyiko lote litampiga mawe. BIBLIA KISWAHILI Mtoe huyo aliyelaani nje ya kambi; na wale wote waliomsikia na waweke mikono yao kichwani mwake, kisha mkutano wote na wamwue kwa kumpiga kwa mawe. |
mkawaketishe watu wawili, watu walaghai, ili wamshitaki, na kumshuhudia, kunena, Umemtukana Mungu na mfalme. Kisha mchukueni nje, mkampige kwa mawe, ili afe.
Kwa siku zote ambazo pigo litakuwa ndani yake atakuwa najisi, ataishi kwa upweke katika makazi yake, nje ya kambi.
Tena uwaambie wana wa Israeli, Mtu yeyote miongoni mwa wana wa Israeli, au miongoni mwa wageni waishio katika Israeli, atakayetoa katika kizazi chake na kumpa Moleki, sharti atauawa; wenyeji wa nchi watampiga kwa mawe.
Tena mwanamume au mwanamke aliye na pepo, au aliye mchawi, hakika atauawa; watawapiga kwa mawe; damu yao itakuwa juu yao.
ndipo umchukue nje malangoni kwako, yule mtu mume, au yule mwanamke, aliyefanya jambo lile ovu; ukawapige kwa mawe, wafe.
Mikono ya wale mashahidi na iwe juu yake kwanza kwa kumwua, kisha mikono ya watu wote. Uondoe vivyo hivyo uovu katikati yako.
Wanaume wote wa mji wake na wamtupie mawe, afe; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako; na Israeli wote watasikia na kuogopa.
na wamtoe nje yule kijana mlangoni pa nyumba ya baba yake, na wanaume wa mji wake wampige kwa mawe hata afe; kwa vile alivyofanya upumbavu katika Israeli, kwa kufanya ukahaba katika nyumba ya baba yake; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako.
Yoshua akasema, Mbona umetufadhaisha hivi? BWANA atakufadhaisha wewe leo. Ndipo Israeli wote wakampiga kwa mawe, kisha wakawateketeza kwa moto, na kuwapiga kwa mawe.