Na mwanamume mwenye govi asiyetahiriwa nyama ya govi lake, mtu yule atatengwa na watu wake; amelivunja agano langu.
Walawi 23:29 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa kuwa mtu yeyote asiyejinyima siku iyo hiyo, atatengwa na watu wake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtu yeyote asiyefunga siku hiyo ni lazima atengwe mbali na watu wake. Biblia Habari Njema - BHND Mtu yeyote asiyefunga siku hiyo ni lazima atengwe mbali na watu wake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtu yeyote asiyefunga siku hiyo ni lazima atengwe mbali na watu wake. Neno: Bibilia Takatifu Mtu ambaye hatafunga siku hiyo ni lazima akatiliwe mbali na watu wake. Neno: Maandiko Matakatifu Mtu yeyote ambaye hatafunga siku hiyo ni lazima akatiliwe mbali na watu wake. BIBLIA KISWAHILI Kwa kuwa mtu yeyote asiyejinyima siku hiyo hiyo, atatengwa na watu wake. |
Na mwanamume mwenye govi asiyetahiriwa nyama ya govi lake, mtu yule atatengwa na watu wake; amelivunja agano langu.
Ndipo nikaamuru kufunga, hapo penye mto Ahava, ili tupate kujinyenyekeza mbele za Mungu, na kutafuta kwake njia iliyonyoka, kwa ajili yetu sisi wenyewe, na kwa ajili ya watoto wetu, na kwa mali yetu yote.
Mtu yeyote atakayechanganya mafuta mfano wa haya, au mtu yeyote atakayetia mafuta haya juu ya mgeni, mtu huyo atatengwa mbali na watu wake.
Siku hiyo Bwana, BWANA wa majeshi, akawaita watu walie na kuomboleza, na kung'oa nywele zao, na kuvaa nguo za magunia;
Watakuja kwa kulia, na kwa maombi nitawaongoza; nitawapitisha kwenye mito ya maji, katika njia iliyonyoka; katika njia hiyo hawatajikwaa; maana mimi ni baba wa Israeli, na Efraimu ni mzaliwa wa kwanza wangu.
Lakini watakaokimbia watakimbia, nao watakuwa juu ya milima kama hua wa bondeni, wote wakilia, kila mmoja katika uovu wake.
Kwa siku zote ambazo pigo litakuwa ndani yake atakuwa najisi, ataishi kwa upweke katika makazi yake, nje ya kambi.
Lakini siku ya kumi ya mwezi huo wa saba ni siku ya upatanisho; itakuwa kusanyiko takatifu kwenu, nanyi mtajinyima; na mtatoa sadaka kwa BWANA kwa njia ya moto.
Na mtu yeyote afanyaye kazi ya namna yoyote siku hiyo, mtu huyo nitamwangamiza atoke katika watu wake.
Itakuwa kwenu sabato ya kustarehe kabisa, nanyi mtajinyima; siku ya tisa ya mwezi wakati wa jioni, tangu jioni hadi jioni, mtaishika hiyo Sabato yenu.
lakini mtu huyo atakayekula katika nyama ya sadaka za amani, ambazo ni za BWANA, na unajisi wake akiwa nao juu yake, mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake.
Kisha mtu awaye yote atakapogusa kitu chochote kilicho najisi, uchafu wa binadamu, au mnyama aliye najisi, au machukizo yoyote yaliyo najisi, kisha akala nyama ya dhabihu ya sadaka za amani, ambazo ni za BWANA, mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake.
Waamrishe wana wa Israeli kwamba wamtoe kila mwenye ukoma kambini, na kila mtu aliye na kisonono, na kila aliye najisi kwa ajili ya maiti;
Na itakuwa ya kwamba kila mtu asiyemsikiliza nabii huyo ataangamizwa na kutengwa na watu wake.