Walawi 22:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na binti ya kuhani ikiwa ameolewa na mgeni, asile katika sadaka ya kuinuliwa katika vitu vile vitakatifu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kama binti yake kuhani ameolewa na mtu asiye kuhani, haruhusiwi kula sadaka ya vitu vitakatifu. Biblia Habari Njema - BHND Kama binti yake kuhani ameolewa na mtu asiye kuhani, haruhusiwi kula sadaka ya vitu vitakatifu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kama binti yake kuhani ameolewa na mtu asiye kuhani, haruhusiwi kula sadaka ya vitu vitakatifu. Neno: Bibilia Takatifu Ikiwa binti ya kuhani ameolewa na mtu asiye kuhani, binti huyo haruhusiwi kula chochote cha matoleo matakatifu. Neno: Maandiko Matakatifu Ikiwa binti wa kuhani ameolewa na mtu asiye kuhani, binti huyo haruhusiwi kula chochote cha matoleo matakatifu. BIBLIA KISWAHILI Na binti ya kuhani ikiwa ameolewa na mgeni, asile katika sadaka ya kuinuliwa katika vitu vile vitakatifu. |
na kwa ajili ya dada yake aliye mwanamwali, aliye wa udugu kwake, ambaye hajaolewa na mwanamume; ana ruhusa kujitia unajisi kwa ajili yake huyo.
Lakini kuhani akinunua mtu yeyote kwa fedha zake, yeye atakula katika hicho; na hao waliozaliwa nyumbani mwake watakula katika chakula chake.
Lakini ikiwa binti ya kuhani ni mjane, au ameachwa na mumewe, wala hana mtoto, kisha amerudi na kuishi katika nyumba ya baba yake, kama vile katika ujana wake, yeye atakula katika chakula cha baba yake; lakini mgeni yeyote asile katika chakula hicho.