Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Walawi 21:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Kwa hiyo basi utamtakasa; kwa kuwa yeye husongeza chakula cha Mungu wako; atakuwa mtakatifu kwako wewe; kwa kuwa mimi BWANA niwatakasaye ninyi ni mtakatifu.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Utamtambua kuhani kuwa aliyewekwa wakfu, maana yeye ndiye anayetoa sadaka ya mkate wa Mungu wako; utamtambua kuwa mtakatifu, maana mimi Mwenyezi-Mungu ninayekuweka wewe wakfu, ni mtakatifu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Utamtambua kuhani kuwa aliyewekwa wakfu, maana yeye ndiye anayetoa sadaka ya mkate wa Mungu wako; utamtambua kuwa mtakatifu, maana mimi Mwenyezi-Mungu ninayekuweka wewe wakfu, ni mtakatifu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Utamtambua kuhani kuwa aliyewekwa wakfu, maana yeye ndiye anayetoa sadaka ya mkate wa Mungu wako; utamtambua kuwa mtakatifu, maana mimi Mwenyezi-Mungu ninayekuweka wewe wakfu, ni mtakatifu.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Waoneni kuwa watakatifu, kwa sababu ndio wanaotoa chakula cha Mungu wenu. Kumbukeni kuwa ni watakatifu, kwa sababu Mimi Mwenyezi Mungu ni mtakatifu, Mimi niwafanyaye ninyi kuwa watakatifu.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Waoneni kuwa watakatifu, kwa sababu ndio wanaotoa chakula cha Mungu wenu. Kumbukeni kuwa ni watakatifu, kwa sababu Mimi bwana ni mtakatifu, Mimi niwafanyaye ninyi kuwa watakatifu.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Kwa hiyo basi utamtakasa; kwa kuwa yeye husongeza chakula cha Mungu wako; atakuwa mtakatifu kwako wewe; kwa kuwa mimi BWANA niwatakasaye ninyi, ni mtakatifu.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Walawi 21:8
18 Marejeleo ya Msalaba  

Uwakumbuke, Ee Mungu wangu, jinsi walivyounajisi ukuhani, na agano la ukuhani na la Walawi.


BWANA akamwambia Musa, Nenda kwa watu hawa, ukawatakase leo na kesho, wakazifue nguo zao,


Musa akateremka mlimani akawaendea watu akawatakasa, nao wakafua nguo zao.


Nawe mvike huyo nduguyo Haruni na wanawe nao mavazi hayo; nawe watie mafuta, na kuwaweka kwa kazi takatifu, na kuwatakasa, ili wapate kunitumikia mimi katika kazi ya ukuhani.


Nawe uwafanyie jambo hili, ili kuwaweka wakfu, wapate kunitumikia mimi katika kazi ya ukuhani; twaa njeku mmoja, na kondoo dume wawili wasio na dosari,


Nena na mkutano wote wa wana wa Israeli, uwaambie, Mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi BWANA, Mungu wenu, ni mtakatifu.


Watakuwa watakatifu kwa Mungu wao, wala wasilinajisi jina la Mungu wao; kwa kuwa wao ndio wasongezao sadaka za BWANA kwa njia ya moto, chakula cha Mungu wao; kwa ajili ya hayo watakuwa watakatifu.


hata wakawatwika ule uovu uletao hatia, hapo walapo vitu vyao vitakatifu; kwa kuwa mimi ndimi BWANA niwatakasaye.


Naye kuhani atayateketeza kwa moto juu ya madhabahu; ni chakula cha dhabihu ya kusongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto.


Mnatoa chakula kilichotiwa unajisi juu ya madhabahu yangu Nanyi mwasema, Sisi tumekutia unajisi kwa jinsi gani? Kwa sababu mwasema, Meza ya BWANA ni kitu cha kudharauliwa.


Waagize hao wana wa Israeli, uwaambie, Matoleo yangu, chakula changu cha sadaka zangu zisongezwazo kwa moto, za harufu ya kupendeza kwangu mimi, mtaangalia kuzisongeza kwangu wakati wake upasao.


je! Yeye ambaye Baba alimtakasa, akamtuma ulimwenguni, ninyi mnamwambia, Unakufuru; kwa sababu nilisema, Mimi ni Mwana wa Mungu?


Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli.


Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?


Maana ilitupasa sisi tuwe na kuhani mkuu wa namna hii aliye mtakatifu, asiyekuwa na uovu, asiyekuwa na waa lolote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu kuliko mbingu;