Walinzi wake ni vipofu, wote pia hawana maarifa; wote ni mbwa walio bubu, hawawezi kulia; huota ndoto, hulala, hupenda usingizi.
Walawi 21:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa kuwa mtu aliye na kasoro ya kimwili hatakaribia, asiyeoana, aliyelemaa mguu au mtu aliyejeruhika uso, au kiungo kilichozidi vimpasavyo mwili, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtu yeyote mwenye dosari sikaribie kunitolea sadaka: Awe kipofu, aliyelemaa, aliyeharibika uso, mwenye kiungo kirefu kuliko kawaida, Biblia Habari Njema - BHND Mtu yeyote mwenye dosari sikaribie kunitolea sadaka: Awe kipofu, aliyelemaa, aliyeharibika uso, mwenye kiungo kirefu kuliko kawaida, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtu yeyote mwenye dosari sikaribie kunitolea sadaka: awe kipofu, aliyelemaa, aliyeharibika uso, mwenye kiungo kirefu kuliko kawaida, Neno: Bibilia Takatifu Hakuna mtu mwenye dosari yoyote awezaye kukaribia: hakuna mtu aliye kipofu au kiwete, au aliyeharibika uso au asiye na viungo kamili, Neno: Maandiko Matakatifu Hakuna mtu mwenye dosari yoyote awezaye kukaribia: hakuna mtu aliye kipofu au kiwete, au aliyeharibika uso au asiye na viungo kamili, BIBLIA KISWAHILI Kwa kuwa mtu aliye na kasoro ya kimwili hatakaribia, asiyeona, aliyelemaa mguu au mtu aliyejeruhika uso, au kiungo kilichozidi kiupasavyo mwili, |
Walinzi wake ni vipofu, wote pia hawana maarifa; wote ni mbwa walio bubu, hawawezi kulia; huota ndoto, hulala, hupenda usingizi.
Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi.
Kwa maana kuna wengi wasiotii, wenye maneno yasiyo na maana, wadanganyaji, na hasa wale wa tohara, ambao yapasa wazibwe vinywa vyao.
Maana imempasa askofu awe mtu asiyeshitakiwa neno, kwa kuwa ni wakili wa Mungu; asiwe mtu wa kujipendeza nafsi yake, asiwe mwepesi wa hasira, asiwe mlevi wala mgomvi, asiwe mpenda mapato ya aibu;