Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Walawi 21:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Nena na Haruni, umwambie, Mtu yeyote wa vizazi vyenu vyote aliye na kilema asikaribie kutoa chakula cha Mungu wake.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

“Mwambie Aroni hivi: Mzawa wako yeyote katika vizazi vyote vijavyo ambaye ana dosari mwilini, haruhusiwi kukaribia na kunitolea mimi Mungu wake sadaka ya mkate.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

“Mwambie Aroni hivi: Mzawa wako yeyote katika vizazi vyote vijavyo ambaye ana dosari mwilini, haruhusiwi kukaribia na kunitolea mimi Mungu wake sadaka ya mkate.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

“Mwambie Aroni hivi: Mzawa wako yeyote katika vizazi vyote vijavyo ambaye ana dosari mwilini, haruhusiwi kukaribia na kunitolea mimi Mungu wake sadaka ya mkate.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

“Mwambie Haruni: ‘Kwa vizazi vijavyo, hakuna mzao wako mwenye dosari atakayekaribia kutoa chakula cha Mungu wake.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

“Mwambie Haruni: ‘Kwa vizazi vijavyo, hakuna mzao wako mwenye dosari atakayekaribia kutoa chakula cha Mungu wake.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Nena na Haruni, umwambie, Mtu yeyote wa vizazi vyenu vyote aliye na kilema asikaribie kutoa chakula cha Mungu wake.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Walawi 21:17
12 Marejeleo ya Msalaba  

Heri mtu yule umchaguaye, Na kumkaribisha akae nyuani mwako. Na tushibe wema wa nyumba yako, Patakatifu pa hekalu lako.

Ndipo Musa akamwambia Haruni, Jambo hili ni hilo BWANA alilolinena, akisema, Nitatakaswa mimi katika hao wanikaribiao, nami nitatukuzwa mbele ya watu hao wote. Haruni akanyamaza kimya.

Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,

mtu yeyote wa wazawa wa Haruni kuhani aliye na kilema asikaribie kuzisongeza sadaka za BWANA kwa njia ya moto; ana kilema huyo asikaribie kusongeza chakula cha Mungu wake.

Watakuwa watakatifu kwa Mungu wao, wala wasilinajisi jina la Mungu wao; kwa kuwa wao ndio wasongezao sadaka za BWANA kwa njia ya moto, chakula cha Mungu wao; kwa ajili ya hayo watakuwa watakatifu.

Naye kuhani atayateketeza kwa moto juu ya madhabahu; ni chakula cha dhabihu ya kusongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto.

Naye kuhani atayateketeza kwa moto juu ya madhabahu; ni chakula cha dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, iwe harufu ya kupendeza; mafuta yote ni ya BWANA.

kisha akanena na Kora na mkutano wake wote, akawaambia, Asubuhi BWANA ataonesha ni kina nani walio wake, kisha ni nani aliye mtakatifu, tena ni nani atakayemkaribisha kwake; maana, yeye atakayemchagua ndiye atakayemsongeza kwake.

Ninyi ni mashahidi, na Mungu pia, jinsi tulivyokaa kwenu ninyi mnaoamini, kwa utakatifu, na kwa haki, bila kulaumiwa;

Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkarimu, ajuaye kufundisha;

Maana ilitupasa sisi tuwe na kuhani mkuu wa namna hii aliye mtakatifu, asiyekuwa na uovu, asiyekuwa na waa lolote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu kuliko mbingu;