Wala hawataoa wanawake wajane, wala mwanamke aliyeachwa na mume wake; lakini watatwaa mabikira wa wazao wa nyumba ya Israeli, au mjane aliyefiwa na mumewe kuhani.
Walawi 21:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Naye atamwoa mwanamke katika ubikira wake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kuhani mkuu aweza tu kumwoa msichana ambaye ni bikira. Biblia Habari Njema - BHND Kuhani mkuu aweza tu kumwoa msichana ambaye ni bikira. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kuhani mkuu aweza tu kumwoa msichana ambaye ni bikira. Neno: Bibilia Takatifu “ ‘Mwanamke atakayeolewa na kuhani lazima awe bikira. Neno: Maandiko Matakatifu “ ‘Mwanamke kuhani atakayemwoa lazima awe bikira. BIBLIA KISWAHILI Naye atamwoa mwanamke katika ubikira wake. |
Wala hawataoa wanawake wajane, wala mwanamke aliyeachwa na mume wake; lakini watatwaa mabikira wa wazao wa nyumba ya Israeli, au mjane aliyefiwa na mumewe kuhani.
wala asitoke katika mahali patakatifu, wala asipatie unajisi mahali patakatifu pa Mungu wake; kwa kuwa utakaso wa hayo mafuta ya kutiwa ya Mungu wake uko juu yake; mimi ndimi BWANA.
Asitwae mjane, wala mwanamke aliyeachwa na mumewe, wala mwanamke mwenye unajisi, wala kahaba; lakini atamwoa mwanamwali katika watu wake mwenyewe.
Wasimwoe mwanamke aliye kahaba, au huyo aliye mwenye unajisi; wala wasimwoe mwanamke aliyeachwa na mumewe; kwa kuwa yeye kuhani ni mtakatifu kwa Mungu wake.
Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa niliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi.
Hawa ndio wasiojitia unajisi na wanawake, kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana-kondoo kila aendako. Hawa wamenunuliwa katika wanadamu, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-kondoo.