Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Walawi 21:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Kisha BWANA akamwambia Musa, Nena na hao makuhani, wana wa Haruni, uwaambie, Mtu asijinajisi kwa ajili ya wafu katika watu wake;

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, “Waambie makuhani, wana wa Aroni, kwamba pasiwe na mtu yeyote miongoni mwao atakayejitia najisi kwa kugusa maiti ya watu wa jamaa yake,

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, “Waambie makuhani, wana wa Aroni, kwamba pasiwe na mtu yeyote miongoni mwao atakayejitia najisi kwa kugusa maiti ya watu wa jamaa yake,

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, “Waambie makuhani, wana wa Aroni, kwamba pasiwe na mtu yeyote miongoni mwao atakayejitia najisi kwa kugusa maiti ya watu wa jamaa yake,

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Sema na makuhani, wana wa Haruni, uwaambie: ‘Kamwe kuhani asijitie unajisi kwa ajili ya mtu wake yeyote anayekufa,

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

bwana akamwambia Musa, “Sema na makuhani, wana wa Haruni, uwaambie: ‘Kamwe kuhani asijitie unajisi kwa utaratibu wa kiibada kwa ajili ya mtu wake yeyote anayekufa,

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Kisha BWANA akamwambia Musa, Nena na hao makuhani, wana wa Haruni, uwaambie, Mtu asijinajisi kwa ajili ya wafu katika watu wake;

Tazama sura
Tafsiri zingine

Walawi 21:1
12 Marejeleo ya Msalaba  

Wala hawatakaribia maiti na kujitia unajisi; ila kwa ajili ya baba, au mama, au mtoto wa kiume, au wa kike, au ndugu mwanamume, au ndugu mwanamke asiyeolewa bado, waweza kujitia unajisi.

Sikieni haya, enyi makuhani, sikilizeni, enyi nyumba ya Israeli, tegeni masikio yenu, enyi wa nyumba ya mfalme, kwa kuwa hukumu hii yawahusu ninyi; maana mmekuwa mtego huko Mizpa, na wavu uliotandwa juu ya Tabori.

Msichanje chale yoyote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi BWANA.

wala hataingia penye maiti, wala asijitie unajisi kwa ajili ya baba yake wala mama yake;

Na sasa, enyi makuhani, amri hii yawahusu ninyi.

Nanyi mtajua ya kuwa mimi nimewaleteeni amri hii, ili agano langu liwe na Lawi, asema BWANA wa majeshi.

Mtu agusaye maiti yeyote atakuwa najisi muda wa siku saba;

Hii ndiyo amri, mtu afapo ndani ya hema; kila mtu aingiaye ndani ya hema hiyo, na kila mtu aliye humo hemani, atakuwa najisi muda wa siku saba.

Kisha mtu yeyote huko nje shambani atakayemgusa mtu aliyeuawa kwa upanga, au mzoga, au mfupa wa mtu, au kaburi, atakuwa najisi muda wa siku saba.

Waamrishe wana wa Israeli kwamba wamtoe kila mwenye ukoma kambini, na kila mtu aliye na kisonono, na kila aliye najisi kwa ajili ya maiti;

Siku hizo zote ambazo alijiweka awe wa BWANA asikaribie maiti.