Walawi 20:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nanyi msiende kwa kuzifuata desturi za taifa, niitoayo mbele yenu; kwa kuwa wao waliyafanya mambo hayo yote, na kwa ajili ya hayo niliwachukia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Msizifuate desturi za taifa ninalolifukuza mbele yenu; kwani waliyafanya hayo yote, nami nikawachukia sana. Biblia Habari Njema - BHND Msizifuate desturi za taifa ninalolifukuza mbele yenu; kwani waliyafanya hayo yote, nami nikawachukia sana. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Msizifuate desturi za taifa ninalolifukuza mbele yenu; kwani waliyafanya hayo yote, nami nikawachukia sana. Neno: Bibilia Takatifu Kamwe msiishi kwa kufuata desturi za mataifa nitakayoyafukuza mbele yenu. Kwa sababu walifanya mambo haya yote, nilichukizwa sana nao. Neno: Maandiko Matakatifu Kamwe msiishi kwa kufuata desturi za mataifa nitakayoyafukuza mbele yenu. Kwa sababu walifanya mambo haya yote, nami nikachukizwa sana nao. BIBLIA KISWAHILI Nanyi msiende kwa kuzifuata desturi za taifa, nilitoalo mbele yenu; kwa kuwa wao waliyafanya mambo hayo yote, na kwa ajili ya hayo niliwachukia. |
Msijitie unajisi katika hata mojawapo ya mambo hayo; kwa maana hayo mataifa nitakayoyatoa mbele zenu yamekuwa najisi kwa mambo hayo yote;
nayo nchi ikawa najisi; na nikaipatiliza kwa ajili ya uovu wake, kisha ikawatema wakazi wake.
(kwa kuwa hao watu wa nchi wameyafanya machukizo haya yote, hao waliotangulia mbele zenu, na hiyo nchi imekuwa najisi;)
Nanyi msifanye matendo kama yale ya nchi ya Misri mlikokaa; wala msifanye matendo kama yale ya nchi ya Kanaani, nitakayowapeleka; wala msifuate amri zao hao.
Kwa hiyo yafuateni maagizo yangu, ili kamwe msiwe na mojawapo ya tabia hizi zinazochukiza, zilizotangulia kufanywa mbele zenu; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
Nami nikawakatilia mbali wachungaji watatu katika mwezi mmoja; maana nafsi yangu ilikuwa imechoka kwa ajili yao, na nafsi zao pia walinichukia.
Si kwa haki yako, wala kwa unyofu wa moyo wako, hivi uingiavyo kuimiliki nchi yao; lakini ni kwa uovu wa mataifa haya BWANA, Mungu wako, awafukuza nje mbele yako; tena apate kuliweka imara hilo neno BWANA alilowaapia baba zako Abrahamu, na Isaka, na Yakobo.