Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Walawi 20:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Basi zishikeni amri zangu zote, na maagizo yangu yote, na kuzifanya; ili kwamba hiyo nchi, ambayo nawapeleka ninyi kukaa, isiwatapike.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

“Mnapaswa kushika na kutekeleza masharti na maagizo yangu yote; la sivyo nchi ile ambamo ninawapeleka itawatapika.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

“Mnapaswa kushika na kutekeleza masharti na maagizo yangu yote; la sivyo nchi ile ambamo ninawapeleka itawatapika.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

“Mnapaswa kushika na kutekeleza masharti na maagizo yangu yote; la sivyo nchi ile ambamo ninawapeleka itawatapika.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

“ ‘Zishikeni amri na sheria zangu zote na kuzifuata, ili nchi ninayowaleta kuishi isiwatapike.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

“ ‘Zishikeni amri na sheria zangu zote na kuzifuata, ili nchi ninayowaleta kuishi isiwatapike.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Basi zishikeni amri zangu zote, na maagizo yangu yote, na kuzifanya; ili kwamba hiyo nchi, ambayo nawapeleka ninyi kukaa, isiwatapike.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Walawi 20:22
20 Marejeleo ya Msalaba  

Ili wazishike amri zake, na kuzitii sheria zake. Haleluya.

Nimeapa nami nikathibitisha, Kuzishika hukumu zako za haki.

Nimeita kwa moyo wangu wote; Ee BWANA, uitike; Nitazishika amri zako.

Jumla ya neno lako ni kweli, Na kila hukumu ya haki yako ni ya milele.

Mara saba kila siku nakusifu, Kwa sababu ya hukumu za haki yako.

Midomo yangu na itoe sifa, Kwa kuwa unanifundisha mausia yako.

Nafsi yangu na iishi, ipate kukusifu, Na hukumu zako zinisaidie.

Roho yangu imepondeka kwa kutamani Hukumu zako kila wakati.

Moyo wangu na uwe mkamilifu katika amri zako, Nisije mimi nikaaibika.

Basi hukumu utakazoziweka mbele ya watu ni hizi

Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.

Zishikeni sheria zangu, na hukumu zangu, na kuzitenda. Mimi ndimi BWANA.

Nanyi nitawatapanyatapanya katika mataifa, nami nitaufuta upanga nyuma yenu; na nchi yenu itakuwa ni ukiwa, na miji yenu maganjo.

haya ndiyo maagizo, amri na hukumu, Musa alizowaambia wana wa Israeli walipotoka Misri;

Musa akawaita Israeli wote, akawaambia, Enyi Israeli, zisikieni amri na hukumu nisemazo masikioni mwenu leo, mpate kujifunza na kuzizingatia.