Mtu yeyote atakayechanganya mafuta mfano wa haya, au mtu yeyote atakayetia mafuta haya juu ya mgeni, mtu huyo atatengwa mbali na watu wake.
Walawi 20:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Tena mwanamume akilala na mwanamke aliye na ugonjwa wake, na kufunua utupu wake; amefunua jito la damu yake, naye mwanamke amefunua jito la damu yake; wote wawili watatengwa mbali na watu wao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kama mwanamume akilala na mwanamke aliye mwezini, wote wawili ni lazima watengwe na watu wao; huyo mwanamume amelala na mwanamke aliye na hedhi, na huyo mwanamke amelala na mwanamume akiwa na hedhi. Biblia Habari Njema - BHND Kama mwanamume akilala na mwanamke aliye mwezini, wote wawili ni lazima watengwe na watu wao; huyo mwanamume amelala na mwanamke aliye na hedhi, na huyo mwanamke amelala na mwanamume akiwa na hedhi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kama mwanamume akilala na mwanamke aliye mwezini, wote wawili ni lazima watengwe na watu wao; huyo mwanamume amelala na mwanamke aliye na hedhi, na huyo mwanamke amelala na mwanamume akiwa na hedhi. Neno: Bibilia Takatifu “ ‘Ikiwa mwanaume atakutana kimwili na mwanamke aliye katika hedhi yake, amefunua mtiririko wa hedhi yake, naye huyo mwanamke amejifunua uchi wake. Wote wawili lazima wakatiliwe mbali na watu wao. Neno: Maandiko Matakatifu “ ‘Ikiwa mwanaume atalala na mwanamke aliye katika hedhi yake na kukutana naye kimwili, amefunua mtiririko wa hedhi yake, naye huyo mwanamke amejifunua uchi wake. Wote wawili lazima wakatiliwe mbali na watu wao. BIBLIA KISWAHILI Tena mwanamume akilala na mwanamke aliye na ugonjwa wake, na kufunua utupu wake; amefunua jito la damu yake, naye mwanamke amefunua jito la damu yake; wote wawili watatengwa mbali na watu wao. |
Mtu yeyote atakayechanganya mafuta mfano wa haya, au mtu yeyote atakayetia mafuta haya juu ya mgeni, mtu huyo atatengwa mbali na watu wake.
hakula juu ya milima, wala hakuviinulia macho vinyago vya nyumba ya Israeli, wala hakumtia unajisi mke wa jirani yake, wala hakumkaribia mwanamke wakati wa kutengwa kwake;
Ndani yako wamefunua uchi wa baba zao; ndani yako wamemfanyia nguvu mwanamke asiye safi wakati wa kutengwa kwake.
Nena na hao wana wa Israeli, uwaambie, Mwanamke akitunga mimba na kuzaa mtoto wa kiume, ndipo atakuwa najisi siku saba; kama katika siku za kutengwa kwake kwa ajili ya hedhi ndivyo atakavyokuwa najisi.
Na mtu yeyote atakayelala na mwanamke na unajisi ukawa juu yake, atakuwa najisi muda wa siku saba; na kila kitanda alichokilalia kitakuwa najisi.