na sheria, na hukumu, na torati, na amri, alizowaandikia, hizo ndizo mtakazozishika na kuzifanya hata milele; wala msiche miungu mingine.
Walawi 19:37 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Zishikeni sheria zangu, na hukumu zangu, na kuzitenda. Mimi ndimi BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ni lazima kuyashika na kuyatekeleza masharti yangu na maagizo yangu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.” Biblia Habari Njema - BHND Ni lazima kuyashika na kuyatekeleza masharti yangu na maagizo yangu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ni lazima kuyashika na kuyatekeleza masharti yangu na maagizo yangu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.” Neno: Bibilia Takatifu “ ‘Shika amri zangu zote na sheria zangu zote, nawe uzifuate. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’ ” Neno: Maandiko Matakatifu “ ‘Shika amri zangu zote na sheria zangu zote, nawe uzifuate. Mimi ndimi bwana.’ ” BIBLIA KISWAHILI Zishikeni sheria zangu, na hukumu zangu, na kuzitenda. Mimi ndimi BWANA. |
na sheria, na hukumu, na torati, na amri, alizowaandikia, hizo ndizo mtakazozishika na kuzifanya hata milele; wala msiche miungu mingine.
Mtazishika amri zangu. Usiwaache wanyama wako wa mfugo wakazaana kwa namna mbalimbali; usipande shamba lako mbegu za namna mbili pamoja; wala usivae mwilini mwako nguo ya namna mbili zilizochanganywa pamoja.
Mizani ya haki, vipimo vya haki, efa ya haki, hini ya haki, ndivyo mtakavyokuwa navyo. Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, niliyewatoa katika nchi ya Misri.
Musa akawaita Israeli wote, akawaambia, Enyi Israeli, zisikieni amri na hukumu nisemazo masikioni mwenu leo, mpate kujifunza na kuzizingatia.
Amri hii ninayokuamuru leo mtaizingatia, mpate kuishi na kuongezeka, na kuingia katika nchi ile ambayo BWANA aliwaapia baba zenu; nanyi mtaimiliki.