tena kazi ya mikate ya wonyesho, na ya unga mwembamba wa sadaka ya unga; ikiwa ni wa maandazi yasiyochachwa, au wa yale yaliyotokoswa, au wa yale yaliyookwa; na kazi ya kila namna ya kipimo na cheo;
Walawi 19:35 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Msifanye yasiyo haki katika hukumu, wala katika kupima, wala katika mizani, wala katika cheo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Usikose kamwe kuamua kwa haki kuhusu vipimo vya urefu, uzito na ujazo. Biblia Habari Njema - BHND “Usikose kamwe kuamua kwa haki kuhusu vipimo vya urefu, uzito na ujazo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Usikose kamwe kuamua kwa haki kuhusu vipimo vya urefu, uzito na ujazo. Neno: Bibilia Takatifu “ ‘Usitumie vipimo vya udanganyifu unapopima urefu, kupima uzito, wala kupima wingi. Neno: Maandiko Matakatifu “ ‘Usitumie vipimo vya udanganyifu unapopima urefu, kupima uzito, wala kupima wingi. BIBLIA KISWAHILI Msifanye yasiyo haki katika hukumu, wala katika kupima, wala katika mizani, wala katika cheo. |
tena kazi ya mikate ya wonyesho, na ya unga mwembamba wa sadaka ya unga; ikiwa ni wa maandazi yasiyochachwa, au wa yale yaliyotokoswa, au wa yale yaliyookwa; na kazi ya kila namna ya kipimo na cheo;
Msitende yasiyo haki katika hukumu, usimpendelee mtu maskini, wala kumstahi mwenye nguvu; bali utamhukumu jirani yako kwa haki.
Basi sasa, sikieni asemavyo BWANA; Simama, ujitetee mbele ya milima, vilima navyo na visikie sauti yako.
Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa.
Uwe na jiwe timilifu la haki, uwe na kipimo kitimilifu cha haki; zipate kuwa nyingi siku zako, katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako.