Na hawa ni wana wa Sibeoni, Aya, na Ana; ni yule Ana aliyeona chemchemi za maji ya moto katika jangwa, alipokuwa akichunga punda za Sibeoni babaye.
Walawi 19:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mtazishika amri zangu. Usiwaache wanyama wako wa mfugo wakazaana kwa namna mbalimbali; usipande shamba lako mbegu za namna mbili pamoja; wala usivae mwilini mwako nguo ya namna mbili zilizochanganywa pamoja. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Yakupasa kuyashika masharti yangu. Usiiache mifugo yako ipandwe na wanyama wa aina nyingine. Shambani mwako usipande mbegu za aina mbili. Usivae vazi lililofumwa kwa aina mbili za nguo. Biblia Habari Njema - BHND “Yakupasa kuyashika masharti yangu. Usiiache mifugo yako ipandwe na wanyama wa aina nyingine. Shambani mwako usipande mbegu za aina mbili. Usivae vazi lililofumwa kwa aina mbili za nguo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Yakupasa kuyashika masharti yangu. Usiiache mifugo yako ipandwe na wanyama wa aina nyingine. Shambani mwako usipande mbegu za aina mbili. Usivae vazi lililofumwa kwa aina mbili za nguo. Neno: Bibilia Takatifu “ ‘Mtazishika amri zangu. “ ‘Usiwaache mifugo wako wakazaana na wa aina tofauti. “ ‘Usipande mbegu za aina mbili katika shamba lako. “ ‘Usivae vazi lililofumwa kwa nyuzi za aina mbili tofauti. Neno: Maandiko Matakatifu “ ‘Mtazishika amri zangu. “ ‘Usiwaache wanyama wako wa kufugwa wakazaana na wengine wa aina tofauti. “ ‘Usipande mbegu za aina mbili katika shamba lako. “ ‘Usivae nguo iliyofumwa kwa nyuzi za aina mbili tofauti. BIBLIA KISWAHILI Mtazishika amri zangu. Usiwaache wanyama wako wa kufugwa wakazaana kwa namna mbalimbali; usipande shamba lako mbegu za namna mbili pamoja; wala usivae mwilini mwako nguo ya namna mbili zilizochanganywa pamoja. |
Na hawa ni wana wa Sibeoni, Aya, na Ana; ni yule Ana aliyeona chemchemi za maji ya moto katika jangwa, alipokuwa akichunga punda za Sibeoni babaye.
Basi watumishi wa Absalomu wakamfanyia Amnoni kama alivyoamuru Absalomu. Ndipo wakaondoka wana wote wa mfalme, wakapanda kila mtu nyumbu wake, wakakimbia.
Na kwa bahati Absalomu akakutana na watumishi wa Daudi. Naye Absalomu alikuwa amepanda nyumbu wake, na yule nyumbu akapita chini ya matawi manene ya mwaloni mkubwa, hata kichwa chake kikakwama katika mwaloni huo, akanyakuliwa juu kati ya mbingu na nchi; na yule nyumbu aliyekuwa chini yake akaenda mbele.
Naye mfalme akawaambia, Twaeni pamoja nanyi watumishi wa bwana wenu, mkampandishe Sulemani mwanangu juu ya nyumbu wangu mimi mkamteremshe mpaka Gihoni;
Farasi wao walikuwa mia saba thelathini na sita; nyumbu wao, mia mbili arubaini na watano;
Mtayatii maagizo yangu, na mtazishika amri zangu, ili kuzifuata; mimi ndimi BWANA Mungu wenu.
Kwa sababu hii zitendeni amri zangu, mkazishike hukumu zangu, na kuzifanya; nanyi mtakaa katika hiyo nchi salama.
Akawaambia na mithali, Hakuna akataye kiraka cha vazi jipya na kukitia katika vazi kuukuu; na kama akitia, amelikata lile jipya, na kile kiraka cha vazi jipya hakilingani na lile vazi kuukuu.
Na sasa, Ee Israeli, zisikilizeni amri na hukumu ninazowafundisha, ili mzitende; mpate kuishi na kuingia na kuimiliki nchi anayowapa BWANA, Mungu wa baba zenu.
Angalieni nimewafundisha amri na hukumu, vile vile kama BWANA, Mungu wangu, alivyoniamuru, ili mzitende katika nchi mwingiayo ili kuimiliki.