Na mahanithi walikuwako katika nchi, wakafanya sawasawa na machukizo yote ya mataifa BWANA aliowafukuza mbele ya wana wa Israeli.
Walawi 18:26 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa hiyo mtazishika amri zangu na maagizo yangu, wala msifanye mojawapo ya machukizo hayo; yeye aliye mzaliwa, wala mgeni aishiye kati yenu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini nyinyi na wageni wanaokaa kati yenu ni lazima kuyashika masharti na maagizo yangu na wala msifanye machukizo hayo. Biblia Habari Njema - BHND Lakini nyinyi na wageni wanaokaa kati yenu ni lazima kuyashika masharti na maagizo yangu na wala msifanye machukizo hayo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini nyinyi na wageni wanaokaa kati yenu ni lazima kuyashika masharti na maagizo yangu na wala msifanye machukizo hayo. Neno: Bibilia Takatifu Lakini ni lazima mzitunze amri zangu na sheria zangu. Wazawa na wageni wanaoishi miongoni mwenu kamwe wasifanye mambo yoyote ya machukizo haya, Neno: Maandiko Matakatifu Lakini ni lazima uzitunze amri zangu na sheria zangu. Mzawa na wageni waishio miongoni mwenu kamwe wasifanye mambo yoyote ya machukizo haya, BIBLIA KISWAHILI Kwa hiyo mtazishika amri zangu na maagizo yangu, wala msifanye mojawapo ya machukizo hayo; yeye aliye mzaliwa, wala mgeni aishiye kati yenu; |
Na mahanithi walikuwako katika nchi, wakafanya sawasawa na machukizo yote ya mataifa BWANA aliowafukuza mbele ya wana wa Israeli.
Kisha mtu yeyote wa nyumba ya Israeli, au miongoni mwa hao wageni wakaao kati yao, atakayekula damu, ya aina yoyote, nitamkataa mtu huyo alaye damu, na nitamtenga na watu wake.
Nawe utawaambia, Mtu yeyote katika nyumba ya Israeli, au miongoni mwa wageni, wanaokaa nao, atoaye sadaka ya kuteketezwa au dhabihu,
nayo nchi ikawa najisi; na nikaipatiliza kwa ajili ya uovu wake, kisha ikawatema wakazi wake.
(kwa kuwa hao watu wa nchi wameyafanya machukizo haya yote, hao waliotangulia mbele zenu, na hiyo nchi imekuwa najisi;)
Kwa hiyo yafuateni maagizo yangu, ili kamwe msiwe na mojawapo ya tabia hizi zinazochukiza, zilizotangulia kufanywa mbele zenu; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
Kwa ajili ya hayo mtazishika amri zangu na maagizo yangu yeyote atakayefanya hivyo ataishi; mimi ndimi BWANA.
Na zile penye udongo mzuri, ndio wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao hulisikia neno, na kulishika; kisha huzaa matunda kwa kuvumilia.
Basi, zishike sheria zake, na amri zake, ninazokuamuru leo, upate kufanikiwa, wewe na watoto wako baada yako, na siku zako ziwe nyingi katika nchi ile akupayo BWANA, Mungu wako, milele.