Naye akamjibu, La, sivyo, ndugu yangu, usinilazimishe; kwani haifai kutendeka hivi katika Israeli; usitende upumbavu huu.
Walawi 18:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Utupu wa binti ya mkewe baba yako, aliyezaliwa na baba yako, yeye ni dada yako, usifunue utupu wake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kamwe usilale na msichana aliyezaliwa na mama yako wa kambo aliyeolewa na baba yako; msichana huyo ni dada yako. Biblia Habari Njema - BHND Kamwe usilale na msichana aliyezaliwa na mama yako wa kambo aliyeolewa na baba yako; msichana huyo ni dada yako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kamwe usilale na msichana aliyezaliwa na mama yako wa kambo aliyeolewa na baba yako; msichana huyo ni dada yako. Neno: Bibilia Takatifu “ ‘Usikutane kimwili na binti ya mke wa baba yako, aliyezaliwa na baba yako; huyo ni dada yako. Neno: Maandiko Matakatifu “ ‘Usikutane kimwili na binti wa mke wa baba yako, aliyezaliwa na baba yako; huyo ni dada yako. BIBLIA KISWAHILI Utupu wa binti ya mkewe baba yako, aliyezaliwa na baba yako, yeye ni dada yako, usifunue utupu wake. |
Naye akamjibu, La, sivyo, ndugu yangu, usinilazimishe; kwani haifai kutendeka hivi katika Israeli; usitende upumbavu huu.
Utupu wa binti ya mwanao wa kiume, au wa binti ya binti yako, utupu wao hao usifunue; kwa kuwa ni utupu wako mwenyewe.
Utupu wa dada yako, binti ya baba yako, au binti ya mama yako, awe alizaliwa nyumbani mwenu au kwingine, utupu wa hao usifunue.