Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika. Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki Atawafanya wengi kuwa wenye haki; Naye atayachukua maovu yao.
Walawi 17:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Lakini iwapo hazifui, wala haogi mwili, ndipo atakapolipizwa uovu wake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini asipoyafua mavazi yake na kuoga, ni lazima mtu huyo awajibike kwa uovu wake.” Biblia Habari Njema - BHND Lakini asipoyafua mavazi yake na kuoga, ni lazima mtu huyo awajibike kwa uovu wake.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini asipoyafua mavazi yake na kuoga, ni lazima mtu huyo awajibike kwa uovu wake.” Neno: Bibilia Takatifu Lakini kama hakufua nguo zake na kuoga, atakuwa na hatia kwa kosa hilo.’ ” Neno: Maandiko Matakatifu Lakini kama hakufua nguo zake na kuoga, atakuwa na hatia kwa kosa hilo.’ ” BIBLIA KISWAHILI Lakini iwapo hazifui, wala haogi mwili, ndipo atakapolipizwa uovu wake. |
Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika. Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki Atawafanya wengi kuwa wenye haki; Naye atayachukua maovu yao.
lakini kila mtu atakayekula atalipizwa uovu wake mwenyewe, kwa sababu amekinajisi kitu hicho kitakatifu cha BWANA; na mtu huyo atatengwa na watu wake.
Tena mwanamume akimwoa dada yake, binti ya baba yake, au binti ya mama yake, na kuuona utupu wake, na huyo mwanamke kauona utupu wake huyo mwanamume; ni jambo la aibu; watengwa mbele ya macho ya wana wa watu wao; amefunua utupu wa dada yake; naye atauchukua uovu wake.
Na mtu yeyote akifanya dhambi, kwa kuwa ameisikia sauti yenye kuapisha, naye akawa ni shahidi, kwamba aliona au kujua, asipolifunua neno lile, ndipo atakapochukua uovu wake mwenyewe;
Tena kama nyama yoyote katika hiyo dhabihu yake ya sadaka za amani ikiliwa siku ya tatu, haitakubaliwa, wala haitahesabiwa kwake huyo mwenye kuisongeza; itakuwa ni machukizo, na mtu atakayeila atachukua uovu wake.
Petro akamwambia, Wewe hutaniosha miguu kamwe. Yesu akamwambia, Nisipokuosha, huna shirika nami.
kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu.
Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.