Nanyi mtakuwa najisi kwa wanyama hao; kila atakayegusa mzoga wao atakuwa ni najisi hata jioni;
Walawi 15:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mtu yeyote atakayekigusa chochote ambacho huyo mwanamke amekalia atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hadi jioni. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtu yeyote atakayegusa kitu chochote anachokalia mwanamke huyo ni lazima ayafue mavazi yake na kuoga kwa maji, naye atakuwa najisi mpaka jioni. Biblia Habari Njema - BHND Mtu yeyote atakayegusa kitu chochote anachokalia mwanamke huyo ni lazima ayafue mavazi yake na kuoga kwa maji, naye atakuwa najisi mpaka jioni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtu yeyote atakayegusa kitu chochote anachokalia mwanamke huyo ni lazima ayafue mavazi yake na kuoga kwa maji, naye atakuwa najisi mpaka jioni. Neno: Bibilia Takatifu Yeyote atakayegusa chochote atakachokalia ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi hadi jioni. Neno: Maandiko Matakatifu Yeyote atakayegusa chochote atakachokalia ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi mpaka jioni. BIBLIA KISWAHILI Mtu yeyote atakayekigusa chochote ambacho huyo mwanamke amekalia atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hadi jioni. |
Nanyi mtakuwa najisi kwa wanyama hao; kila atakayegusa mzoga wao atakuwa ni najisi hata jioni;
Mtu yeyote atakayekigusa kitanda chake huyo mwanamke atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hadi jioni.
Kiwe ni katika kitanda, au chochote alichokikalia huyo mwanamke, atakapokigusa kitu hicho, atakuwa najisi hadi jioni.
Na kitu chochote atakachokigusa mtu aliye najisi kitakuwa najisi; na mtu atakayekigusa kitu hicho atakuwa najisi hadi jioni.