Walawi 15:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na kitu chochote ambacho anakalia katika kutengwa kwake kitakuwa najisi; na kila kitu ambacho amekalia kitakuwa najisi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kitu chochote anacholalia au kukalia wakati yu najisi, kitakuwa najisi. Biblia Habari Njema - BHND Kitu chochote anacholalia au kukalia wakati yu najisi, kitakuwa najisi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kitu chochote anacholalia au kukalia wakati yu najisi, kitakuwa najisi. Neno: Bibilia Takatifu “ ‘Chochote atakacholalia wakati wake wa hedhi kitakuwa najisi, na chochote atakachokikalia kitakuwa najisi. Neno: Maandiko Matakatifu “ ‘Chochote atakacholalia wakati wake wa hedhi kitakuwa najisi, na chochote atakachokikalia kitakuwa najisi. BIBLIA KISWAHILI Na kitu chochote ambacho anakalia katika kutengwa kwake kitakuwa najisi; na kila kitu ambacho amekalia kitakuwa najisi. |
Nami nimeona lililo na uchungu kupita mauti; yaani, mwanamke ambaye moyo wake ni mitego na tanzi, na mikono yake ni kama vifungo; yeye ampendezaye Mungu atamponyoka, bali mwenye dhambi atanaswa na yeye.
Mwanamke yeyote aliye na hedhi, atatengwa kwa muda wa siku saba; na mtu yeyote atakayemgusa atakuwa najisi hadi jioni.
Mtu yeyote atakayekigusa kitanda chake huyo mwanamke atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hadi jioni.