Nyavu zao hazitakuwa mavazi, wala hawatajifunika kwa kazi zao; kazi zao ni kazi za uovu, na vitendo vya udhalimu vimo mikononi mwao.
Walawi 13:47 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kuhusu mavazi; vazi ambalo pigo la ukoma limo ndani yake, liwe ni vazi la sufu au la katani; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Kama kuna namna ya upele wa ukoma kwenye vazi, liwe la sufu au kitani, Biblia Habari Njema - BHND “Kama kuna namna ya upele wa ukoma kwenye vazi, liwe la sufu au kitani, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Kama kuna namna ya upele wa ukoma kwenye vazi, liwe la sufu au kitani, Neno: Bibilia Takatifu “Kuhusu vazi lolote lililoharibiwa na maambukizo ya ukoma, liwe ni vazi la sufu au kitani, Neno: Maandiko Matakatifu “Kama vazi lolote lina maambukizo ya upele: likiwa ni vazi la sufu au kitani, BIBLIA KISWAHILI Kuhusu mavazi; vazi ambalo pigo la ukoma limo ndani yake, liwe ni vazi la sufu au la katani; |
Nyavu zao hazitakuwa mavazi, wala hawatajifunika kwa kazi zao; kazi zao ni kazi za uovu, na vitendo vya udhalimu vimo mikononi mwao.
Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu, na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi; sisi sote twanyauka kama jani, na maovu yetu yatuondoa, kama upepo uondoavyo.
Ukatwaa baadhi ya mavazi yako, ukajifanyia mahali palipoinuka, palipopambwa kwa rangi mbalimbali, ukafanya mambo ya kikahaba juu yake; mambo kama hayo hayatakuja wala hayatakuwako.
Kwa siku zote ambazo pigo litakuwa ndani yake atakuwa najisi, ataishi kwa upweke katika makazi yake, nje ya kambi.
likiwa limefumwa, au kusokotwa; likiwa ni la kitani au la sufu; liwe katika ngozi, au kitu chochote kilichofanywa cha ngozi;
Naye ataliteketeza vazi hilo, liwe ni la kufumwa au ni la kusokotwa, kama ni la sufu, au la kitani, au kitu chochote cha ngozi, ambacho kina hilo pigo ndani yake; kwa maana, ni ukoma unaona; vazi hilo litateketezwa;
Na katika pigo la ukoma katika vazi la sufu, au la kitani, kama ni katika lililofumwa, au lililosokotwa, au katika kitu chochote cha ngozi, sheria yake ni hiyo, kusema kwamba ni safi, au kusema kwamba ni najisi.
Usiku umeendelea sana, mchana umekaribia, basi na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru.
mvue mwenendo wenu wa kwanza, utu wa zamani unaoharibika, kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya;
na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto; na wengine wahurumieni kwa hofu, mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili.