Akakwea kutoka huko mpaka Betheli; naye alipokuwa akienda njiani, wakatoka vijana katika mji, wakamfanyizia mzaha, wakamwambia, Paa wewe mwenye upaa! Paa wewe mwenye upaa!
Walawi 13:40 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwamba nywele za mtu zimemtoka kichwani mwake, yeye ni mwenye upara, ni safi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Kama mwanamume amepata upara, yeye ni safi kwani ana upara tu. Biblia Habari Njema - BHND “Kama mwanamume amepata upara, yeye ni safi kwani ana upara tu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Kama mwanamume amepata upara, yeye ni safi kwani ana upara tu. Neno: Bibilia Takatifu “Wakati mwanaume hana nywele naye ana upara, yeye ni safi. Neno: Maandiko Matakatifu “Wakati mwanaume hana nywele naye ana upaa, yeye ni safi. BIBLIA KISWAHILI Kwamba nywele za mtu zimemtoka kichwani mwake, yeye ni mwenye upara, ni safi. |
Akakwea kutoka huko mpaka Betheli; naye alipokuwa akienda njiani, wakatoka vijana katika mji, wakamfanyizia mzaha, wakamwambia, Paa wewe mwenye upaa! Paa wewe mwenye upaa!
Wanapanda juu hata Bayithi na Diboni, mpaka mahali palipo juu ili walie; juu ya Nebo na juu ya Medeba Wamoabi wanalia; Wana upaa juu ya vichwa vyao vyote; kila ndevu zimenyolewa.
ndipo kuhani ataangalia; ikiwa vile vipaku ving'aavyo vilivyo katika ngozi ya mwili wake ni vyeupe kidogo; ni mba iliyotokeza katika ngozi; yeye ni safi.
Tena kwamba nywele za mtu zimemtoka kichwani upande wa mbele, yeye ni mwenye upara wa kipaji; ni safi.
Nami nitazigeuza sikukuu zenu kuwa maombolezo, na nyimbo zenu zote kuwa vilio; nami nitatia nguo za magunia katika viuno vyote, na upara katika kila kichwa; nami nitayafanya haya kuwa kama maombolezo kwa ajili ya mwana wa pekee, na mwisho wake kama siku ya uchungu.
Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake;
Nasema kwa jinsi ya kibinadamu kwa sababu ya udhaifu wa miili yenu. Kwa kuwa kama mlivyovitoa viungo vyenu vitumiwe na uchafu na uasi mpate kuasi, vivyo hivyo sasa vitoeni viungo vyenu vitumiwe na haki mpate kutakaswa.
Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki.
Lakini mwajua ya kuwa niliwahubiria Injili mara ya kwanza kwa sababu ya udhaifu wa mwili;