Mtu atakapokuwa na uvimbe katika ngozi ya mwili wake, au upele, au kipaku king'aacho, nao ukawa ni ugonjwa wa ukoma katika ngozi ya mwili wake, ndipo atakapoletwa kwa Haruni kuhani, au kwa mmojawapo wa wanawe makuhani;
Walawi 13:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC na kuhani atamwangalia siku ya saba; kama kimeenea katika ngozi, ndipo huyo kuhani atasema kuwa ni najisi; hili ni pigo la ukoma. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Siku ya saba kuhani atamwangalia. Kama umeenea kwenye ngozi, basi, kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa najisi; kwani anao ugonjwa wa ukoma. Biblia Habari Njema - BHND Siku ya saba kuhani atamwangalia. Kama umeenea kwenye ngozi, basi, kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa najisi; kwani anao ugonjwa wa ukoma. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Siku ya saba kuhani atamwangalia. Kama umeenea kwenye ngozi, basi, kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa najisi; kwani anao ugonjwa wa ukoma. Neno: Bibilia Takatifu Siku ya saba kuhani atamchunguza tena, na kama unaenea kwenye ngozi, kuhani atamtangaza kuwa najisi; ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza. Neno: Maandiko Matakatifu Siku ya saba kuhani atamchunguza tena, na kama unaenea kwenye ngozi, kuhani atamtangaza kuwa najisi; ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza. BIBLIA KISWAHILI na kuhani atamwangalia siku ya saba; kama kimeenea katika ngozi, ndipo huyo kuhani atasema kuwa ni najisi; hili ni pigo la ukoma. |
Mtu atakapokuwa na uvimbe katika ngozi ya mwili wake, au upele, au kipaku king'aacho, nao ukawa ni ugonjwa wa ukoma katika ngozi ya mwili wake, ndipo atakapoletwa kwa Haruni kuhani, au kwa mmojawapo wa wanawe makuhani;
Lakini kuhani akipaangalia, nywele nyeupe hamna katika hicho kipaku king'aacho, nacho hakikuingia ndani kuliko ngozi, lakini chafifia; ndipo kuhani atamweka mahali muda wa siku saba;
Na kama hicho kipaku kikibaki pale pale, wala hakikuenea katika ngozi, lakini kimefifia; ni kufura kwake pale penye moto, na kuhani atasema kuwa ni safi; kwa kuwa ni kovu la kuwasha hili.
Lakini ikiwa kipele kimeenea katika ngozi yake baada ya kujionesha kwa kuhani ili kutakaswa, atamwendea kuhani tena;
siku ya saba kuhani atakwenda tena, naye ataangalia; na tazama, likiwa pigo limeenea katika kuta za nyumba;