Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuimiliki; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
Walawi 12:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nena na hao wana wa Israeli, uwaambie, Mwanamke akitunga mimba na kuzaa mtoto wa kiume, ndipo atakuwa najisi siku saba; kama katika siku za kutengwa kwake kwa ajili ya hedhi ndivyo atakavyokuwa najisi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Waambie watu wa Israeli hivi: Mwanamke akipata mimba, akajifungua mtoto wa kiume, atakuwa najisi kwa muda wa siku saba kulingana na siku zake zihusikanazo na hali ya wanawake. Biblia Habari Njema - BHND “Waambie watu wa Israeli hivi: Mwanamke akipata mimba, akajifungua mtoto wa kiume, atakuwa najisi kwa muda wa siku saba kulingana na siku zake zihusikanazo na hali ya wanawake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Waambie watu wa Israeli hivi: Mwanamke akipata mimba, akajifungua mtoto wa kiume, atakuwa najisi kwa muda wa siku saba kulingana na siku zake zihusikanazo na hali ya wanawake. Neno: Bibilia Takatifu “Waambie Waisraeli: ‘Mwanamke ambaye atapata mimba na kuzaa mtoto wa kiume atakuwa najisi kwa siku saba, kama anavyokuwa najisi wakati wa siku zake za hedhi. Neno: Maandiko Matakatifu “Waambie Waisraeli: ‘Mwanamke ambaye atapata mimba na kuzaa mtoto wa kiume atakuwa najisi kwa kawaida ya ibada kwa siku saba, kama anavyokuwa najisi wakati wa siku zake za hedhi. BIBLIA KISWAHILI Nena na hao wana wa Israeli, uwaambie, Mwanamke akitunga mimba na kuzaa mtoto wa kiume, ndipo atakuwa najisi siku saba; kama katika siku za kutengwa kwake kwa ajili ya hedhi ndivyo atakavyokuwa najisi. |
Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuimiliki; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa uchungu utazaa watoto; hata hivyo, hamu yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.
Basi Daudi akatuma wajumbe, akamtwaa; naye akaingia kwake; naye akalala naye; (maana yule mwanamke amekwisha kutakasika unajisi wake); kisha akarudi nyumbani kwake.
Je! Mwanadamu ni kitu gani, hata akawa safi? Huyo aliyezaliwa na mwanamke, hata awe na haki?
Basi mtu awezaje kuwa na haki mbele ya Mungu? Au awezaje kuwa safi aliyezaliwa na mwanamke?
Lakini kama amezaa mtoto wa kike naye atakaa muda wa siku sitini na sita ili kutakata damu yake.
Mwanamke yeyote aliye na hedhi, atatengwa kwa muda wa siku saba; na mtu yeyote atakayemgusa atakuwa najisi hadi jioni.
au kama akiugusa uchafu wa binadamu, uchafu wowote ambao kwao amepata unajisi, bila kujua, hapo apatapo kulijua, ndipo atakapokuwa na hatia;
Kisha, zilipotimia siku za kutakasika kwao, kama ilivyo Torati ya Musa walikwenda naye hata Yerusalemu, wamweke kwa Bwana,