Wanyama hao ndio walio najisi kwenu katika hao watambaao; yeyote atakayewagusa, wakiisha kuwa mgoza, atakuwa ni najisi hata jioni.
Walawi 11:32 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Tena kitu chochote, wanyama hao mmojawapo atakachokiangukia, wakiisha kufa, kitakuwa ni najisi; cha mti, nguo, ngozi, gunia, chombo chochote cha kufanyia kazi yoyote, lazima kitiwe ndani ya maji, nacho kitakuwa ni najisi hadi jioni; ndipo kitakapokuwa ni safi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ikiwa mzoga wa viumbe hao unakiangukia kitu chochote, kiwe ni kifaa cha mbao au vazi au ngozi au gunia au chombo chochote kitumiwacho kwa kusudi lolote lile, chombo hicho kitakuwa najisi mpaka jioni. Ili kukifanya kiwe safi ni lazima kukiosha kwa maji. Biblia Habari Njema - BHND Ikiwa mzoga wa viumbe hao unakiangukia kitu chochote, kiwe ni kifaa cha mbao au vazi au ngozi au gunia au chombo chochote kitumiwacho kwa kusudi lolote lile, chombo hicho kitakuwa najisi mpaka jioni. Ili kukifanya kiwe safi ni lazima kukiosha kwa maji. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ikiwa mzoga wa viumbe hao unakiangukia kitu chochote, kiwe ni kifaa cha mbao au vazi au ngozi au gunia au chombo chochote kitumiwacho kwa kusudi lolote lile, chombo hicho kitakuwa najisi mpaka jioni. Ili kukifanya kiwe safi ni lazima kukiosha kwa maji. Neno: Bibilia Takatifu Ikiwa mmoja wao atakufa na kuangukia juu ya kitu fulani, chombo hicho, hata kikiwa cha matumizi gani, kitakuwa najisi, kiwe kimetengenezwa kwa mti, nguo, ngozi au gunia. Kiweke ndani ya maji; kitakuwa najisi hadi jioni, kisha kitakuwa safi tena. Neno: Maandiko Matakatifu Ikiwa mmoja wao atakufa na kuangukia juu ya kitu fulani, chombo hicho, hata kikiwa cha matumizi gani, kitakuwa najisi, kiwe kimetengenezwa kwa mti, nguo, ngozi au gunia. Kiweke ndani ya maji; kitakuwa najisi mpaka jioni, kisha kitakuwa safi tena. BIBLIA KISWAHILI Tena kitu chochote, wanyama hao mmojawapo atakachokiangukia, wakiisha kufa, kitakuwa ni najisi; cha mti, nguo, ngozi, gunia, chombo chochote cha kufanyia kazi yoyote, lazima kitiwe ndani ya maji, nacho kitakuwa ni najisi hadi jioni; ndipo kitakapokuwa ni safi. |
Wanyama hao ndio walio najisi kwenu katika hao watambaao; yeyote atakayewagusa, wakiisha kuwa mgoza, atakuwa ni najisi hata jioni.
Tena mtu atakayeingia ndani ya hiyo nyumba wakati huo wote iliofungwa, atakuwa najisi hadi jioni.
Na chombo cha udongo ambacho amekigusa mwenye kisonono, kitavunjwavunjwa; na kila chombo cha mti kitaoshwa majini.
na kuhani atawasongeza, mmoja kuwa sadaka ya dhambi, na wa pili kuwa sadaka ya kuteketezwa; naye kuhani atafanya upatanisho mbele za BWANA kwa ajili ya kisonono chake.
Na mtu yule amwachaye mbuzi wa Azazeli aende zake, ataosha nguo zake, na kuosha mwili wake kwa maji, na baadaye ataingia katika kambi.
Tena kila mtu atakayekula nyamafu, au nyama ya mnyama aliyeraruliwa na wanyama, awe ni mzalia au mgeni, atafua nguo zake, na kuoga majini naye atakuwa najisi hadi jioni; ndipo atakapokuwa safi.
huyo mtu atakayegusa kitu chochote namna hiyo atakuwa najisi hata jioni, naye hatakula katika vitu vitakatifu, asipooga mwili wake majini.
Lakini hicho chombo cha udongo ambacho hiyo nyama ilipikwa ndani yake kitavunjwa; na kama ikipikwa katika chombo cha shaba, kitasuguliwa, na kuoshwa kwa maji.
Ndipo kuhani atazifua nguo zake, na kuoga mwili wake majini, kisha baadaye ataingia kambini, naye kuhani atakuwa najisi hadi jioni.
ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wake mwenyewe walio na bidii katika matendo mema.
si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa mara ya pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu;