Walawi 11:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC katika hao mna ruhusa kuwala; nzige kwa aina zake, na nzige kuu kwa aina zake, na panzi kwa aina zake, na parare kwa aina zake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hao ni: Kila aina ya nzige, kila aina ya senene, kila aina ya panzi na kila aina ya parare. Biblia Habari Njema - BHND Hao ni: Kila aina ya nzige, kila aina ya senene, kila aina ya panzi na kila aina ya parare. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hao ni: kila aina ya nzige, kila aina ya senene, kila aina ya panzi na kila aina ya parare. Neno: Bibilia Takatifu Miongoni mwa hawa, mtakula nzige wa aina zote, senene, parare au panzi. Neno: Maandiko Matakatifu Miongoni mwa hawa, mtakula nzige wa aina zote, senene, parare au panzi. BIBLIA KISWAHILI katika hao mna ruhusa kuwala; nzige kwa aina zake, na nzige kuu kwa aina zake, na panzi kwa aina zake, na parare kwa aina zake. |
Pamoja na hayo, hivi vitambaavyo vyenye mabawa viendavyo kwa miguu minne ni halali kula, hao walio na miguu mirefu, ya kurukia juu ya nchi;
Naye Yohana mwenyewe alikuwa na vazi lake la singa za ngamia, na mshipi wa ngozi kiunoni mwake; na chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni.
Na Yohana alikuwa amevaa singa za ngamia na mshipi wa ngozi kiunoni mwake, akala nzige na asali ya mwituni.
Basi imetupasa sisi tulio na nguvu kuuchukua udhaifu wao wasio na nguvu, wala haitupasi kujipendeza wenyewe.
Yeye ambaye tuna maneno mengi ya kunena kuhusu habari zake; na ni shida kuyaeleza kwa kuwa mmekuwa wavivu wa kusikia.