Wakolosai 4:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba mkiwa na shukrani; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Dumuni katika sala, na mnaposali muwe waangalifu, mkimshukuru Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Dumuni katika sala, na mnaposali muwe waangalifu, mkimshukuru Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Dumuni katika sala, na mnaposali muwe waangalifu, mkimshukuru Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Dumuni sana katika maombi, mkikesha katika hayo pamoja na kushukuru. Neno: Maandiko Matakatifu Dumuni sana katika maombi, mkikesha katika hayo pamoja na kushukuru. BIBLIA KISWAHILI Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba mkiwa na shukrani; |
Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.
Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kusali, pamoja nao wanawake, na Mariamu mama yake Yesu, na ndugu zake.
kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;
Msijisumbue kwa neno lolote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.
Kwa sababu hiyo sisi nasi, tangu siku ile tuliposikia, hatuachi kufanya maombi na dua kwa ajili yenu, ili mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni;
wenye shina na wenye kujengwa katika yeye; mmefanywa imara kwa imani, kama mlivyofundishwa; mkizidi kutoa shukrani.
Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani.
Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kupitia kwake.
Epafra, aliye mtu wa kwenu, mtumwa wa Yesu Kristo, awasalimu, akifanya bidii siku zote kwa ajili yenu katika maombi yake, ili msimame mkiwa wakamilifu na kuthibitika kabisa katika mapenzi yote ya Mungu.
Lakini mimi, hasha! Nisimtende BWANA dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi; lakini nitawaelimisha katika njia iliyo njema, na kunyoka