Isaka akamwingiza Rebeka katika hema ya mama yake, Sara, akamtwaa Rebeka, akawa mkewe, akampenda; Isaka akafarijika kwa ajili ya kufa kwa mama yake.
Wakolosai 3:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nanyi waume, wapendeni wake zenu, na msiwe wakali kwao. Biblia Habari Njema - BHND Nanyi waume, wapendeni wake zenu, na msiwe wakali kwao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nanyi waume, wapendeni wake zenu, na msiwe wakali kwao. Neno: Bibilia Takatifu Ninyi waume, wapendeni wake zenu, wala msiwe wakali kwao. Neno: Maandiko Matakatifu Ninyi waume, wapendeni wake zenu, wala msiwe na uchungu dhidi yao. BIBLIA KISWAHILI Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao. |
Isaka akamwingiza Rebeka katika hema ya mama yake, Sara, akamtwaa Rebeka, akawa mkewe, akampenda; Isaka akafarijika kwa ajili ya kufa kwa mama yake.
Uishi kwa furaha pamoja na mke umpendaye, siku zote za maisha yako ya ubatili, ulizopewa chini ya jua; siku zote za ubatili wako, kwa maana hiyo ni sehemu yako ya maisha; na katika kazi zako unazozifanya chini ya jua.
Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake wa kiume na wa kike; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matusi yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya;
Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda kanisa, akajitoa kwa ajili yake;
Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mumewe.
Lakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu, wala msiseme uongo juu ya kweli.
Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; maana wao pia ni warithi wa neema ya uzima, ili maombi yenu yasizuiliwe na chochote.