Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa uchungu utazaa watoto; hata hivyo, hamu yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.
Wakolosai 3:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ninyi wake, watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Enyi wake, watiini waume zenu, kwani ndivyo apendavyo Bwana. Biblia Habari Njema - BHND Enyi wake, watiini waume zenu, kwani ndivyo apendavyo Bwana. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Enyi wake, watiini waume zenu, kwani ndivyo apendavyo Bwana. Neno: Bibilia Takatifu Ninyi wake, watiini waume zenu, kama inavyostahili katika Bwana Isa. Neno: Maandiko Matakatifu Ninyi wake, watiini waume zenu, kama inavyostahili katika Bwana Isa. BIBLIA KISWAHILI Ninyi wake, watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana. |
Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa uchungu utazaa watoto; hata hivyo, hamu yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.
Basi mbiu ya mfalme atakayoipiga itakapotangazwa katika ufalme wake wote, nao ni mkubwa, wake wote watawaheshimu waume zao, wakubwa kwa wadogo.
Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu.
Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo.
Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wowote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu;