Wakolosai 2:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na ninyi mmetimilika katika yeye aliye kichwa cha enzi yote na mamlaka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema nanyi mmepewa uhai kamili katika kuungana naye. Yeye yuko juu ya pepo watawala wote na wakuu wote. Biblia Habari Njema - BHND nanyi mmepewa uhai kamili katika kuungana naye. Yeye yuko juu ya pepo watawala wote na wakuu wote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza nanyi mmepewa uhai kamili katika kuungana naye. Yeye yuko juu ya pepo watawala wote na wakuu wote. Neno: Bibilia Takatifu nanyi mmepewa ukamilifu ndani ya Al-Masihi, aliye mkuu juu ya kila nguvu na kila mamlaka. Neno: Maandiko Matakatifu nanyi mmepewa ukamilifu ndani ya Al-Masihi, ambaye ndiye mkuu juu ya kila enzi na kila mamlaka. BIBLIA KISWAHILI Na ninyi mmetimilika katika yeye aliye kichwa cha enzi yote na mamlaka. |
Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.
ili sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho;
na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu.
akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuziaibisha hadharani, akiziongoza kwa ushindi wake wa shangwe.
Hapo hapana Mgiriki wala Myahudi, kutahiriwa wala kutotahiriwa, mgeni wala mshenzi, mtumwa wala muungwana, bali Kristo ni yote, na katika yote.
naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii;
Naye yuko katika mkono wa kulia wa Mungu, amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zikiisha kutiishwa chini yake.