Wagalatia 6:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maana kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maana kila mmoja anapaswa kuubeba mzigo wake mwenyewe. Biblia Habari Njema - BHND Maana kila mmoja anapaswa kuubeba mzigo wake mwenyewe. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maana kila mmoja anapaswa kuubeba mzigo wake mwenyewe. Neno: Bibilia Takatifu Kwa maana, kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa maana, kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe. BIBLIA KISWAHILI Maana kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe. |
Mimi, BWANA, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake.
mkuu wa mashauri, muweza katika kutenda; ambaye macho yake yamefumbuka juu ya njia zote za wanadamu, kumpa kila mtu kwa kadiri ya njia zake, na kwa kadiri ya matunda ya matendo yake,
Tazama, roho zote ni mali yangu; kama vile roho ya baba ni mali yangu, ndivyo ilivyo roho ya mwana mali yangu; roho ile itendayo dhambi itakufa.
Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
Basi yeye apandaye, na yeye atiaye maji ni wamoja, lakini kila mtu atapata thawabu yake mwenyewe kulingana na taabu yake mwenyewe.
Basi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye atayamulika yaliyositirika katika giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.
nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye fikira na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake.
Tazama, naja upesi, na malipo yangu yako pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.