Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.
Wagalatia 5:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tukiishi kwa msaada wa Roho, na tuufuate mwongozo wake. Biblia Habari Njema - BHND Tukiishi kwa msaada wa Roho, na tuufuate mwongozo wake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tukiishi kwa msaada wa Roho, na tuufuate mwongozo wake. Neno: Bibilia Takatifu Kwa kuwa tunaishi kwa Roho wa Mungu, basi, tuenende kwa Roho. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa kuwa tunaishi kwa Roho, basi, tuenende kwa Roho. BIBLIA KISWAHILI Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho. |
Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.
Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki.
Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.
Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa kiumbe aliye hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha.
Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.
Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili.
Maana kwa ajili hiyo hata hao waliokufa walihubiriwa Injili, ili kwamba wahukumiwe katika mwili kama wahukumiwavyo wanadamu; bali wawe hai katika roho kama Mungu alivyo hai.
Na baada ya siku hizo tatu u nusu, roho ya uhai itokayo kwa Mungu ikawaingia, wakasimama kwa miguu yao; na hofu kuu ikawaangukia watu waliowatazama.