Basi Abrahamu alikuwa mzee mwenye miaka mingi, na BWANA alikuwa amembariki Abrahamu katika vitu vyote.
Wagalatia 3:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi hao walio wa imani hubarikiwa pamoja na Abrahamu aliyekuwa mwenye imani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, wale walio na imani wanabarikiwa pamoja na Abrahamu aliyeamini. Biblia Habari Njema - BHND Basi, wale walio na imani wanabarikiwa pamoja na Abrahamu aliyeamini. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, wale walio na imani wanabarikiwa pamoja na Abrahamu aliyeamini. Neno: Bibilia Takatifu Kwa sababu hii, wale wote wanaoamini wanabarikiwa pamoja na Ibrahimu, mtu wa imani. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa sababu hii, wale wote wanaoamini wanabarikiwa pamoja na Ibrahimu, mtu wa imani. BIBLIA KISWAHILI Basi hao walio wa imani hubarikiwa pamoja na Abrahamu aliyekuwa mwenye imani. |
Basi Abrahamu alikuwa mzee mwenye miaka mingi, na BWANA alikuwa amembariki Abrahamu katika vitu vyote.
Naye aliipokea dalili hii ya kutahiriwa, mhuri wa ile haki ya imani aliyokuwa nayo kabla hajatahiriwa; apate kuwa baba yao wote waaminio, ijapokuwa hawakutahiriwa, ili na wao pia wahesabiwe haki;
Kwa hiyo ilitoka katika imani, iwe kwa njia ya neema, ili kwamba ile ahadi iwe imara kwa wazawa wote; si kwa wale wa torati tu, ila na kwa wale wa imani ya Abrahamu; aliye baba yetu sisi sote;
bali na kwa ajili yetu sisi mtakaohesabiwa vivyo hivyo, sisi tunaomwamini yeye aliyemfufua Yesu Bwana wetu katika wafu;
ili kwamba baraka ya Abrahamu iwafikie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani.
Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Abrahamu, na warithi kulingana na ahadi.