Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Wagalatia 3:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Abrahamu.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Sasa basi, jueni kwamba watu wenye kumwamini ndio walio watoto halisi wa Abrahamu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Sasa basi, jueni kwamba watu wenye kumwamini ndio walio watoto halisi wa Abrahamu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Sasa basi, jueni kwamba watu wenye kumwamini ndio walio watoto halisi wa Abrahamu.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Fahamuni basi kwamba wale walio na imani, hao ndio watoto wa Ibrahimu.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Fahamuni basi kwamba wale walio na imani, hao ndio watoto wa Ibrahimu.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Abrahamu.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Wagalatia 3:7
11 Marejeleo ya Msalaba  

Jueni kwamba BWANA ndiye Mungu; Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake; Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake.

Yesu akamwambia, Leo wokovu umefika nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa Abrahamu.

Nanyi kadhalika, mwonapo mambo hayo yanaanza kutokea, tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu u karibu.

Wakajibu, wakamwambia, Baba yetu ndiye Abrahamu! Yesu akawaambia, Kama mngekuwa watoto wa Abrahamu, mngezitenda kazi zake Abrahamu.

bali na kwa ajili yetu sisi mtakaohesabiwa vivyo hivyo, sisi tunaomwamini yeye aliyemfufua Yesu Bwana wetu katika wafu;

Basi hao walio wa imani hubarikiwa pamoja na Abrahamu aliyekuwa mwenye imani.

Na wote watakaoenenda kwa kanuni hiyo, amani na iwe kwao na rehema, naam, kwa Israeli wa Mungu.

Jueni ya kuwa ndugu yetu Timotheo amekwisha kufunguliwa; ambaye, akija upesi, nitaonana nanyi pamoja naye.