Wagalatia 3:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nyinyi nyote mliobatizwa mkaungana na Kristo ni kama vile mmemvaa Kristo. Biblia Habari Njema - BHND Nyinyi nyote mliobatizwa mkaungana na Kristo ni kama vile mmemvaa Kristo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nyinyi nyote mliobatizwa mkaungana na Kristo ni kama vile mmemvaa Kristo. Neno: Bibilia Takatifu Kwa maana wote mliobatizwa ndani ya Al-Masihi, mmemvaa Al-Masihi. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa maana wote mliobatizwa ndani ya Al-Masihi, mmemvaa Al-Masihi. BIBLIA KISWAHILI Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo. |
Nitafurahi sana katika BWANA, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu.
Lakini baba aliwaambia watumwa wake, Lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike; mtieni na pete kidoleni, na viatu miguuni;
Hata alipokwisha kubatizwa, yeye na nyumba yake, akatusihi, akisema, Kama mmeniona kuwa mwaminifu kwa Bwana, ingieni nyumbani mwangu mkakae. Akatusihi sana.
Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu.
ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti;
Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wagiriki; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.
mkivaa utu mpya, unaofanywa upya katika ufahamu kulingana na mfano wake yeye aliyeuumba.
Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi; (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo.