Na habari zake zikaenea katika Shamu yote; wakamletea wote waliokuwa wagonjwa, walioshikwa na maradhi mbalimbali na mateso, wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.
Wagalatia 1:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Baadaye nilikwenda pande za Shamu na Kilikia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Baadaye nilikwenda katika tarafa za Siria na Kilikia. Biblia Habari Njema - BHND Baadaye nilikwenda katika tarafa za Siria na Kilikia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Baadaye nilikwenda katika tarafa za Siria na Kilikia. Neno: Bibilia Takatifu Baadaye nilienda sehemu za Siria na Kilikia. Neno: Maandiko Matakatifu Baadaye nilikwenda sehemu za Syria na Kilikia. BIBLIA KISWAHILI Baadaye nilikwenda pande za Shamu na Kilikia. |
Na habari zake zikaenea katika Shamu yote; wakamletea wote waliokuwa wagonjwa, walioshikwa na maradhi mbalimbali na mateso, wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.
Na huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao ni Barnaba, na Simeoni aitwaye Nigeri, na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa ndugu wa kulelewa wa mfalme Herode, na Sauli.
Mitume na ndugu wazee, kwa ndugu zetu walioko Antiokia na Shamu na Kilikia, walio wa Mataifa; Salamu.
Baada ya hayo Paulo akazidi kukaa huko siku nyingi, kisha akaagana na ndugu akaabiri kwenda Shamu; na Priskila na Akila wakaenda pamoja naye, alipokwisha kunyoa kichwa chake huko Kenkrea; maana alikuwa ana nadhiri.
Na tulipoona Kipro tukaiacha upande wa kushoto; tukasafiri mpaka Shamu tukashuka Tiro. Kwa maana huko ndiko merikebu yetu itakakoshusha shehena yake.
Paulo akasema, Mimi ni mtu wa Kiyahudi, mtu wa Tarso, mji wa Kilikia, mwenyeji wa mji usiokuwa mnyonge. Nakuomba, nipe ruhusa niseme na wenyeji hawa.
Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nilizaliwa Tarso, mji wa Kilikia, ila nililelewa katika mji huu, miguuni pa Gamalieli, nikafundishwa sheria ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa jitihada kubwa kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo leo hivi;
Naye alipokwisha kuisoma, akawauliza, Mtu huyu ni wa mkoa gani? Alipoarifiwa ya kuwa ni mtu wa Kilikia,
Lakini baadhi ya watu wa sinagogi lililoitwa sinagogi la Mahuru, na la Wakirene, na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka na kujadiliana na Stefano;