Wagalatia 1:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Lakini sikumwona mtume mwingine, ila Yakobo, ndugu yake Bwana. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini sikuwaona mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana. Biblia Habari Njema - BHND Lakini sikuwaona mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini sikuwaona mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana. Neno: Bibilia Takatifu Lakini sikumwona mtume mwingine yeyote isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana Isa. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini sikumwona mtume mwingine yeyote isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana Isa. BIBLIA KISWAHILI Lakini sikumwona mtume mwingine, ila Yakobo, ndugu yake Bwana. |
Alipokuwa katika kusema na makutano, tazama, mama yake na ndugu zake walikuwa wakisimama nje, wataka kusema naye.
Huyu si mwana wa seremala? Mamaye si yeye aitwaye Mariamu? Na nduguze si Yakobo, na Yusufu, na Simoni, na Yuda?
na Andrea, na Filipo, na Bartholomayo, na Mathayo, na Tomaso, na Yakobo wa Alfayo, na Thadayo, na Simoni Mkananayo,
Huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu, na ndugu yao Yakobo, na Yose, na Yuda, na Simoni? Na dada zake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake.
Akaletewa habari akiambiwa, Mama yako na ndugu zako wamesimama nje wakitaka kuonana nawe.
Wakati walipoingia, wakapanda ghorofani, walipokuwa wakikaa; Petro, na Yohana, na Yakobo, na Andrea, Filipo na Tomaso, Bartholomayo na Mathayo, Yakobo wa Alfayo, na Simoni Zelote, na Yuda wa Yakobo.
Naye akawapungia mkono wanyamaze, akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa katika gereza. Akasema, Kampasheni Yakobo na wale ndugu habari hizi. Akaondoka, akaenda mahali pengine.
Hatuna uwezo kuchukua pamoja nasi mke aliye ndugu, kama wao mitume wengine, na ndugu wa Bwana, na Kefa?
Yakobo, mtumwa wa Mungu, na wa Bwana Yesu Kristo, kwa makabila kumi na mawili waliotawanyika; salamu.
Yuda, mtumwa wa Yesu Kristo, ndugu yake Yakobo, kwa hao walioitwa, waliopendwa katika Mungu Baba, na kuhifadhiwa kwa ajili ya Yesu Kristo.