Binti wa kimalkia, jinsi ulivyo mzuri Hatua zako katika mitarawanda. Mapaja yako ya mviringo ni kama johari, Kazi ya mikono ya fundi stadi;
Waefeso 6:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC na kama viatu vilivyofungiwa miguuni mwenu muwe tayari kutangaza Injili ya amani; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema na hamu ya kutangaza Habari Njema ya amani iwe kama viatu miguuni mwenu. Biblia Habari Njema - BHND na hamu ya kutangaza Habari Njema ya amani iwe kama viatu miguuni mwenu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza na hamu ya kutangaza Habari Njema ya amani iwe kama viatu miguuni mwenu. Neno: Bibilia Takatifu nayo miguu yenu ivalishwe viatu vya utayari tunaopata katika Injili ya amani. Neno: Maandiko Matakatifu nayo miguu yenu ifungiwe utayari tuupatao kwa Injili ya amani. BIBLIA KISWAHILI na kama viatu vilivyofungiwa miguuni mwenu muwe tayari kutangaza Injili ya amani; |
Binti wa kimalkia, jinsi ulivyo mzuri Hatua zako katika mitarawanda. Mapaja yako ya mviringo ni kama johari, Kazi ya mikono ya fundi stadi;
Jinsi ilivyo mizuri juu ya milima Miguu yake aletaye habari njema, Yeye aitangazaye amani, Aletaye habari njema ya mambo mema, Yeye autangazaye wokovu, Auambiaye Sayuni, Mungu wako anamiliki!
MUNGU, aliye BWANA, ni nguvu zangu, Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu, Naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka.
Lakini baba aliwaambia watumwa wake, Lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike; mtieni na pete kidoleni, na viatu miguuni;
Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!
Makomeo yako yatakuwa ya chuma na shaba; Na kadiri ya siku zako ndivyo zitakavyokuwa nguvu zako.