Basi, nikaweka watu, mahali pa chini pa nafasi iliyokuwa nyuma ya ukuta, mahali palipokuwa wazi, kwa kadiri ya jamaa zao, nikawaweka waliojihami na panga zao, na mikuki yao, na pinde zao.
Waefeso 6:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Vaeni silaha anazowapeni Mungu mpate kuzipinga mbinu mbaya za Ibilisi. Biblia Habari Njema - BHND Vaeni silaha anazowapeni Mungu mpate kuzipinga mbinu mbaya za Ibilisi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Vaeni silaha anazowapeni Mungu mpate kuzipinga mbinu mbaya za Ibilisi. Neno: Bibilia Takatifu Vaeni silaha zote za Mungu ili mweze kuzipinga hila za ibilisi. Neno: Maandiko Matakatifu Vaeni silaha zote za Mwenyezi Mungu ili kwamba mweze kuzipinga hila za ibilisi. BIBLIA KISWAHILI Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. |
Basi, nikaweka watu, mahali pa chini pa nafasi iliyokuwa nyuma ya ukuta, mahali palipokuwa wazi, kwa kadiri ya jamaa zao, nikawaweka waliojihami na panga zao, na mikuki yao, na pinde zao.
kwa maana watajitokeza Makristo wa uongo, na manabii wa uongo, watatoa ishara na maajabu, wapate kuwadanganya, ikiwezekana, hata hao wateule.
Usiku umeendelea sana, mchana umekaribia, basi na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru.
Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita muwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili muweze kustahimili.
(maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)
Lakini nahofu; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo.
ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, wasiione nuru ya Injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.
katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za haki za mkono wa kulia na za mkono wa kushoto;
ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa mafundisho, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.
Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
mkivaa utu mpya, unaofanywa upya katika ufahamu kulingana na mfano wake yeye aliyeuumba.
Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani na upendo, na chapeo yetu iwe tumaini la wokovu.
Naye, kwa sababu hii, anaweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.
Muwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka zunguka, akitafuta mtu ammeze.
Yeye awezaye kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu;
Lile joka kuu likatupwa, yule nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika wake wakatupwa pamoja naye.
Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao hao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wakiwa hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti;
Lakini nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, wowote wasio na mafundisho hayo, wasiozijua fumbo za Shetani, kama vile wasemavyo, Sitaweka juu yenu mzigo mwingine.
ili kwamba vizazi vya wana wa Israeli wapate kujua ili kuwafundisha vita, hasa wao ambao hawakujua vita kabla ya wakati ule;